DAFTARI LA MKUTANO WA HUDUMA NA MAISHA

Msifu Yehova kwa Wimbo

Kiswahili
Msifu Yehova kwa Wimbo
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/202020286/univ/art/202020286_univ_sqr_xl.jpg
mwb20 Agosti uku. 4

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | KUTOKA 15-16

Msifu Yehova kwa Wimbo

Msifu Yehova kwa Wimbo

15:1, 2, 11, 18, 20, 21

Muziki unaweza kuathiri sana jinsi tunavyofikiri na kuhisi. Kuimba ni sehemu muhimu ya ibada yetu kwa Yehova.

  • Musa na Waisraeli walimwimbia Yehova sifa alipowakomboa kimuujiza kwenye Bahari Nyekundu

  • Mfalme Daudi aliwaweka rasmi wanaume 4,000 kuwa waimbaji na wanamuziki hekaluni

  • Yesu na mitume wake walimwimbia Yehova sifa usiku uliotangulia kifo chake

Nina fursa zipi za kumwimbia Yehova sifa?