Yeremia 47:1-7
-
Unabii dhidi ya Wafilisti (1-7)
47 Hili ndilo neno la Yehova kwa nabii Yeremia kuwahusu Wafilisti,+ kabla ya Farao kushambulia Gaza.
2 Yehova anasema hivi:
“Tazama! Maji yanakuja kutoka kaskazini.
Yatakuwa mto unaofurika.
Nayo yataifunika nchi na kila kitu kilichomo,Jiji na wale wanaokaa humo.
Wanaume watalia kwa sauti,Na kila mtu anayeishi katika nchi ataomboleza.
3 Watakaposikia sauti ya kishindo cha kwato za farasi dume wake,Watakaposikia kelele za magari yake ya vitaNa mvumo wa magurudumu yake,Akina baba hata hawatageuka kuwatazama wana wao,Kwa maana mikono yao italegea,
4 Kwa sababu siku inayokuja itawaangamiza Wafilisti wote;+Itamwangamiza kabisa kutoka Tiro+ na kutoka Sidoni+ kila msaidizi aliyebaki.
Kwa maana Yehova atawaangamiza Wafilisti,Ambao wamebaki wa kisiwa cha Kaftori.*+
5 Upara* utakuja Gaza.
Ashkeloni limenyamazishwa.+
Ewe uliyebaki katika bonde lao tambarare,*Utaendelea kujikatakata mpaka lini?+
6 Aha! Upanga wa Yehova!+
Utanyamaza mpaka lini?
Rudi ndani ya ala yako.
Pumzika na unyamaze.
7 Upanga unawezaje kukaa kimyaWakati Yehova ameuamuru?
Ushambulie Ashkeloni na pwani ya bahari,+Hapo ndipo alipoupa kazi.”
Maelezo ya Chini
^ Yaani, Krete.
^ Yaani, watanyoa vichwa vyao kwa kuomboleza na kwa aibu.
^ Au “nchi yao tambarare ya chini.”