Wimbo wa Sulemani 6:1-13

 • Mabinti wa Yerusalemu (1)

 • Msichana (2, 3)

  • “Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu mimi” (3)

 • Mfalme (4-10)

  • “Wewe ni mrembo kama Tirsa” (4)

  • Maneno ya wanawake (10)

 • Msichana (11, 12)

 • Mfalme (na wengine) (13a)

 • Msichana (13b)

 • Mfalme (na wengine) (13c) (na wengine)

6  “Mpenzi wako ameenda wapi,Ewe mwanamke mrembo kuliko wote? Mpenzi wako amegeuka na kufuata njia gani? Acha tukamtafute pamoja nawe.”   “Mpenzi wangu ameshuka kwenda kwenye bustani yake,Kwenye kitalu cha mimea ya viungo,Kuchunga kondoo kwenye bustaniNa kuchuma mayungiyungi.+   Mimi ni wa mpenzi wangu,Na mpenzi wangu ni wangu mimi.+ Anachunga kondoo kati ya mayungiyungi.”+   “Wewe ni mrembo, kama Tirsa,*+ mpenzi wangu,+Unapendeza kama Yerusalemu,+Unavutia sana kama majeshi yaliyokusanyika kuzunguka bendera zao.+   Usinitazame,+Ukinitazama nahangaika. Nywele zako ni kama kundi la mbuziLinaloshuka kwenye miteremko ya Gileadi.+   Meno yako ni kama kundi la kondooAmbao wametoka kuoshwa,Wote wamezaa mapacha,Na hakuna yeyote aliyepoteza watoto wake.   Kama kipande cha komamangaNdivyo yalivyo mashavu yako nyuma ya shela yako.   Hata kukiwa na malkia 60 Na masuria 80 Na wasichana wasiohesabika.+   Lakini kuna mmoja tu ambaye ni njiwa wangu,+ mpenzi wangu asiye na kasoro. Binti pekee kwa mama yake. Yeye ni kipenzi cha mama yake.* Mabinti wanapomwona, humtangaza kuwa mwenye furaha;Malkia na masuria humsifu. 10  ‘Ni mwanamke gani anayeng’aa* kama mapambazuko,Mrembo kama mwezi mpevu,Aliye mwangavu kama nuru ya jua,Mwenye kuvutia sana kama majeshi yaliyokusanyika kuzunguka bendera zao?’”+ 11  “Nilishuka kwenye bustani ya miti yenye kokwa+Ili nione machipukizi bondeni,Nione ikiwa mzabibu umechipuaIkiwa mikomamanga imechanua. 12  Bila kutarajia,Tamaa yangu ilinifikishaKwenye magari ya watu wangu waungwana.”* 13  “Rudi, rudi, ewe Mshulami! Rudi, rudi,Ili tukutazame!” “Kwa nini mnamkodolea macho Mshulami?”+ “Yeye ni kama dansi ya kambi mbili!”*

Maelezo ya Chini

Au “Jiji Linalopendeza.”
Tnn., “ndiye aliye safi sana kwa yule aliyemzaa.”
Tnn., “anayetazama chini.”
Au “watu wangu walio tayari kusaidia.”
Au “dansi ya Mahanaimu.”