Wimbo wa Sulemani 3:1-11

  • Msichana (1-5)

    • ‘Usiku, nilimtafuta ninayempenda’ (1)

  • Mabinti wa Sayuni (6-11)

    • Maelezo kuhusu msafara wa Sulemani

3  “Nyakati za usiku nikiwa kitandani mwangu,Nilimtafuta ninayempenda.*+ Nilimtafuta mwanamume huyo lakini sikumpata.+   Nitaamka na kuzunguka jijini;Barabarani na katika viwanja vya mji,Acheni nimtafute ninayempenda.* Nilimtafuta mwanamume huyo, lakini sikumpata.   Nilikutana na walinzi waliokuwa wakizunguka jijini.+ Nikawauliza, ‘Mmemwona ninayempenda?’*   Mara tu baada ya kuwapitaNilimpata ninayempenda.* Nikamshika na sikumwacha aendeMpaka nilipomleta ndani ya nyumba ya mama yangu,+Katika chumba cha ndani cha aliyenizaa.   Nawaapisha, enyi binti za Yerusalemu,Kwa swala na paa jike wa porini: Msijaribu kuamsha au kuchochea upendo ndani yangu mpaka utakapoamka wenyewe.”+   “Ni nini hiki kinachokuja kutoka nyikani kama nguzo za moshi,Kilicho na manukato ya manemane na ubani,Na manukato yote ya ungaunga yanayouzwa na wafanyabiashara?”+   “Tazameni! Ni kochi la Sulemani. Wanaume sitini mashujaa wanalizunguka,Miongoni mwa wanaume mashujaa wa Israeli,+   Wote wamejihami kwa upanga,Wote wamezoezwa kwa ajili ya vita,Kila mmoja wao ana upanga kiunoniIli akabiliane na mambo yanayotisha wakati wa usiku.”   “Ni kochi la kifahari* la Mfalme SulemaniAlilojitengenezea kwa mbao za Lebanoni.+ 10  Alitengeneza nguzo zake kwa fedha,Viegemeo vyake kwa dhahabu. Kiti chake kwa sufu ya zambarau;Sehemu yake ya ndani ilipambwa kwa upendoNa mabinti wa Yerusalemu.” 11  “Tokeni nje, enyi binti za Sayuni,Mtazameni Mfalme SulemaniAmevaa taji la harusi* ambalo mama yake+ alimtengenezeaSiku yake ya harusi,Siku ambayo moyo wake ulishangilia.”

Maelezo ya Chini

Au “yule ambaye nafsi yangu inampenda.”
Au “yule ambaye nafsi yangu inampenda.”
Au “yule ambaye nafsi yangu inampenda?”
Au “yule ambaye nafsi yangu inampenda.”
Kochi lililofunikwa ambalo lilitumiwa kuwabeba watu mashuhuri.
Au “shada; koja la maua.”