Mambo ya Walawi 11:1-47

  • Wanyama safi na wasio safi (1-47)

11  Kisha Yehova akawaambia Musa na Haruni:  “Waambieni Waisraeli, ‘Hawa ndio wanyama wa nchi kavu mnaoweza kula:+  Mnaweza kumla kila mnyama mwenye kwato zilizopasuka na zilizogawanyika anayecheua.  “‘Lakini hampaswi kuwala wanyama wafuatao wanaocheua au wenye kwato zilizogawanyika: msimle ngamia kwa sababu anacheua lakini kwato zake hazijagawanyika. Yeye si safi kwenu.+  Pia, msimle wibari+ kwa sababu anacheua lakini kwato zake hazijagawanyika. Yeye si safi kwenu.  Pia, msimle sungura kwa sababu anacheua lakini kwato zake hazijagawanyika. Yeye si safi kwenu.  Pia, msimle nguruwe+ kwa sababu ana kwato zilizopasuka na kugawanyika lakini hacheui. Yeye si safi kwenu.  Msile kamwe nyama yao wala kugusa mizoga yao. Hao si safi kwenu.+  “‘Kati ya viumbe wote wanaoishi ndani ya maji, mnaweza kula wafuatao: Mnaweza kumla kiumbe yeyote wa majini mwenye mapezi na magamba anayeishi baharini au mtoni.+ 10  Lakini kiumbe yeyote anayeishi baharini na mtoni ambaye hana mapezi na magamba, kati ya viumbe wote wa majini wanaoishi katika makundi makubwa na viumbe wengine wote wanaoishi majini, ni chukizo kwenu. 11  Naam, watakuwa chukizo kwenu, msile kamwe nyama yao,+ nanyi mnapaswa kuchukia mizoga yao. 12  Kiumbe yeyote wa majini ambaye hana mapezi na magamba ni chukizo kwenu. 13  “‘Hawa ndio ndege mnaopaswa kuchukia; wasiliwe kwa sababu ni chukizo: tai,+ furukombe, tumbusi* mweusi,+ 14  mwewe mwekundu na aina zote za mwewe weusi, 15  kila aina ya kunguru, 16  mbuni, bundi, shakwe, kila aina ya kipanga, 17  bundi mdogo, mnandi, bundi mwenye masikio marefu, 18  batamaji, mwari, tumbusi,* 19  korongo, kila aina ya kulastara, hudihudi, na popo. 20  Kila kiumbe mwenye mabawa* anayeishi katika makundi makubwa anayetambaa kwa miguu yote minne ni chukizo kwenu. 21  “‘Kati ya wadudu wote wenye mabawa wanaoishi katika makundi makubwa na wanaotambaa kwa miguu yote minne, mnaweza kula tu wadudu wenye vifundo miguuni wanaoruka ardhini. 22  Hawa ndio mnaoweza kula: kila aina ya nzige wanaohama, nzige wengine wanaoliwa,+ chenene,* na panzi. 23  Wadudu wengine wote wenye mabawa wanaoishi katika makundi makubwa wenye miguu minne ni chukizo kwenu. 24  Wadudu hao watawafanya msiwe safi. Kila mtu anayegusa mizoga yao hatakuwa safi mpaka jioni.+ 25  Kila mtu anayebeba mizoga yao anapaswa kufua mavazi yake;+ hatakuwa safi mpaka jioni. 26  “‘Mnyama yeyote mwenye kwato zilizopasuka lakini hazijagawanyika na ambaye hacheui si safi kwenu. Kila mtu anayewagusa wanyama hao hatakuwa safi.+ 27  Kila kiumbe anayetembea kwa miguu yenye makucha kati ya viumbe wanaotembea kwa miguu minne si safi kwenu. Kila mtu anayegusa mizoga yao hatakuwa safi mpaka jioni. 28  Yeyote atakayebeba mizoga yao anapaswa kufua mavazi yake,+ hatakuwa safi mpaka jioni.+ Hao si safi kwenu. 29  “‘Hawa ndio viumbe wanaotambaa ambao si safi kwenu: fuko, panya,+ kila aina ya mjusi, 30  mjusi kafiri, mjusi mkubwa, mjusi wa majini, mjusi wa mchangani, na kinyonga. 31  Viumbe hao wanaotambaa si safi kwenu.+ Kila mtu anayegusa mizoga yao hatakuwa safi mpaka jioni.+ 32  “‘Viumbe hao wakifa na kuangukia kitu chochote, kitu hicho hakitakuwa safi, iwe ni chombo cha mbao, nguo, ngozi, au gunia. Chombo chochote kinachotumiwa kinapaswa kutumbukizwa majini, nacho hakitakuwa safi mpaka jioni; baada ya hapo kitakuwa safi. 33  Wakianguka ndani ya chombo cha udongo, mnapaswa kukivunja, na chochote kilichokuwa ndani ya chombo hicho si safi.+ 34  Chakula chochote kinachomwagikiwa na maji kutoka katika chombo hicho si safi, na kinywaji chochote kutoka katika chombo hicho si safi. 35  Kitu chochote kinachoangukiwa na mizoga yao si safi. Vitu hivyo vitavunjwavunjwa iwe ni jiko kubwa au dogo. Vitu hivyo si safi, navyo havitakuwa safi kwenu. 36  Hata hivyo, chemchemi au tangi la maji litabaki safi, lakini mtu yeyote anayegusa mizoga yao hatakuwa safi. 37  Mizoga yao ikiangukia mbegu za kupandwa, zitabaki safi. 38  Lakini mbegu zikitiwa maji kisha sehemu yoyote ya mizoga yao iangukie mbegu hizo, mbegu hizo si safi kwenu. 39  “‘Mnyama yeyote mnayeruhusiwa kula akifa, yeyote anayegusa mzoga wake hatakuwa safi mpaka jioni.+ 40  Yeyote anayekula sehemu yoyote ya mzoga huo anapaswa kufua mavazi yake, hatakuwa safi mpaka jioni.+ Na yeyote anayebeba mzoga huo anapaswa kufua mavazi yake, naye hatakuwa safi mpaka jioni. 41  Kila kiumbe anayetambaa ni chukizo.+ Hapaswi kuliwa. 42  Hampaswi kumla kiumbe yeyote anayetambaa kwa tumbo, kiumbe yeyote anayetembea kwa miguu yote minne, au viumbe wowote wanaoishi katika makundi makubwa wenye miguu mingi, kwa sababu viumbe hao ni chukizo.+ 43  Msinifanye niwachukie kwa kula kiumbe yeyote kati ya viumbe hao, msijitie unajisi na kuwa watu wasio safi.+ 44  Kwa maana mimi ni Yehova Mungu wenu,+ nanyi lazima mjitakase na kuwa watakatifu,+ kwa sababu mimi ni mtakatifu.+ Kwa hiyo msijichafue kwa kula kiumbe yeyote anayetambaa. 45  Kwa maana mimi ni Yehova, ninayewaongoza kupanda kutoka nchini Misri ili nijithibitishe mwenyewe kuwa Mungu wenu,+ nanyi lazima muwe watakatifu,+ kwa sababu mimi ni mtakatifu.+ 46  “‘Hiyo ndiyo sheria kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe anayeishi majini, na kila kiumbe anayetambaa, 47  ili kutofautisha viumbe walio safi na wasio safi na viumbe wanaoweza kuliwa na wasioweza kuliwa.’”+

Maelezo ya Chini

Au “tai mla mizoga.”
Au “tai mla mizoga.”
Au “Kila mdudu.”
Au “nyenje.”