Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kitabu cha Kumbukumbu la Torati

Sura

Muhtasari wa Yaliyomo

 • 1

  • Kuondoka Mlima Horebu (1-8)

  • Wakuu na waamuzi wawekwa (9-18)

  • Watu wakosa kutii kule Kadesh-barnea (19-46)

   • Waisraeli wakataa kuingia katika ile nchi (26-33)

   • Washindwa kuteka Kanaani (41-46)

 • 2

  • Kutangatanga nyikani kwa miaka 38 (1-23)

  • Wamshinda Mfalme Sihoni wa Heshboni (24-37)

 • 3

  • Wamshinda Mfalme Ogu wa Bashani (1-7)

  • Kugawanywa kwa nchi upande wa mashariki wa Yordani (8-20)

  • Yoshua aambiwa asiogope (21, 22)

  • Musa hataingia katika nchi hiyo (23-29)

 • 4

  • Waagizwa watii (1-14)

   • Msisahau matendo ya Mungu (9)

  • Yehova anataka aabudiwe yeye peke yake (15-31)

  • Hakuna Mungu mwingine ila Yehova (32-40)

  • Majiji ya makimbilio upande wa mashariki wa Yordani (41-43)

  • Wapewa Sheria (44-49)

 • 5

  • Agano la Yehova kule Horebu (1-5)

  • Amri Kumi zarudiwa (6-22)

  • Watu waogopa kwenye Mlima Sinai (23-33)

 • 6

  • Mpende Yehova kwa moyo wako wote (1-9)

   • “Sikilizeni, enyi Waisraeli” (4)

   • Wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto (6, 7)

  • Msimsahau Yehova (10-15)

  • Msimjaribu Yehova (16-19)

  • Kiambieni kizazi kinachofuata (20-25)

 • 7

  • Mataifa saba yataangamizwa (1-6)

  • Sababu ya Waisraeli kuchaguliwa (7-11)

  • Utii utawaletea mafanikio wakati ujao (12-26)

 • 8

  • Baraka kutoka kwa Yehova zatajwa tena (1-9)

   • “Haishi kwa mkate tu” (3)

  • Msimsahau Yehova (10-20)

 • 9

  • Sababu ya Waisraeli kupewa ile nchi (1-6)

  • Waisraeli wamkasirisha Yehova mara nne (7-29)

   • Ndama wa dhahabu (7-14)

   • Musa aingilia kati (15-21, 25-29)

   • Wamkasirisha mara tatu zaidi (22)

 • 10

  • Mabamba mawili yatengenezwa tena (1-11)

  • Analotaka Yehova (12-22)

   • Mwogopeni na kumpenda Yehova (12)

 • 11

  • Mmeuona ukuu wa Yehova (1-7)

  • Nchi Iliyoahidiwa (8-12)

  • Thawabu za kutii (13-17)

  • Maneno ya Mungu yakaziwe katika mioyo (18-25)

  • “Baraka na laana” (26-32)

 • 12

  • Abuduni mahali ambapo Mungu amechagua (1-14)

  • Waruhusiwa kula nyama lakini si damu (15-28)

  • Msinaswe na miungu mingine (29-32)

 • 13

  • Jinsi ya kuwatendea waasi imani (1-18)

 • 14

  • Njia zisizofaa za kuomboleza (1, 2)

  • Vyakula safi na visivyo safi (3-21)

  • Sehemu ya kumi kwa ajili ya Yehova (22-29)

 • 15

  • Madeni yafutwa kila mwaka wa saba (1-6)

  • Kuwasaidia maskini (7-11)

  • Kuwaachilia huru watumwa kila mwaka wa saba (12-18)

   • Kutoboa sikio la mtumwa kwa msumari (16, 17)

  • Wazaliwa wa kwanza wa wanyama watakaswa (19-23)

 • 16

  • Pasaka; Sherehe ya Mikate Isiyo na Chachu (1-8)

  • Sherehe ya Majuma (9-12)

  • Sherehe ya Vibanda (13-17)

  • Kuwaweka waamuzi (18-20)

  • Vitu vya ibada vilivyokatazwa (21, 22)

 • 17

  • Dhabihu zisiwe na kasoro (1)

  • Kushughulikia uasi imani (2-7)

  • Kuamua kesi ngumu (8-13)

  • Maagizo kwa ajili ya mfalme atakayetawala (14-20)

   • Mfalme aandike nakala ya Sheria (18)

 • 18

  • Fungu la makuhani na Walawi (1-8)

  • Mazoea ya kuwasiliana na roho waovu yakatazwa (9-14)

  • Nabii kama Musa (15-19)

  • Jinsi ya kuwatambua manabii wa uwongo (20-22)

 • 19

  • Hatia ya damu na majiji ya makimbilio (1-13)

  • Alama za mipaka zisisogezwe (14)

  • Mashahidi mahakamani (15-21)

   • Mashahidi wawili au watatu wahitajika (15)

 • 20

  • Sheria za vita (1-20)

   • Wale ambao hawakuruhusiwa kwenda vitani (5-9)

 • 21

  • Mauaji yaliyofanywa na watu wasiojulikana (1-9)

  • Kuoa wanawake mateka (10-14)

  • Haki ya mzaliwa wa kwanza (15-17)

  • Mwana mkaidi (18-21)

  • Mtu aliyetundikwa mtini amelaaniwa (22, 23)

 • 22

  • Kuheshimu wanyama wa jirani (1-4)

  • Kuvaa nguo za watu wa jinsia tofauti (5)

  • Kuwatendea wanyama kwa fadhili (6, 7)

  • Ukuta unaozunguka ukingo wa paa (8)

  • Michanganyiko isiyofaa (9-11)

  • Vishada vya nguo (12)

  • Sheria kuhusu kukiuka maadili ya ngono (13-30)

 • 23

  • Wasioruhusiwa katika kutaniko la Mungu (1-8)

  • Usafi wa kambi (9-14)

  • Watumwa waliokimbia (15, 16)

  • Ukahaba wakatazwa (17, 18)

  • Riba na nadhiri (19-23)

  • Vitu ambavyo wapita njia wanaruhusiwa kula (24, 25)

 • 24

  • Ndoa na talaka (1-5)

  • Kuheshimu uhai (6-9)

  • Kuwajali maskini (10-18)

  • Sheria kuhusu kuokota masalio (19-22)

 • 25

  • Sheria kuhusu kumpiga mtu viboko (1-3)

  • Usimfunge kinywa ng’ombe dume anapopura (4)

  • Ndoa ya ndugu mkwe (5-10)

  • Kumkamata mtu sehemu zisizofaa anapopigana (11, 12)

  • Mizani na vipimo sahihi (13-16)

  • Waamaleki wataangamizwa (17-19)

 • 26

  • Kutoa mavuno ya kwanza (1-11)

  • Sehemu ya kumi iliyotolewa mara ya pili (12-15)

  • Waisraeli ni mali ya pekee ya Yehova (16-19)

 • 27

  • Sheria itaandikwa kwenye mawe (1-10)

  • Kwenye Mlima Ebali na Mlima Gerizimu (11-14)

  • Laana zatangazwa (15-26)

 • 28

  • Baraka za kutii (1-14)

  • Laana za kutotii (15-68)

 • 29

  • Agano pamoja na Waisraeli kule Moabu (1-13)

  • Onyo kuhusu kutotii (14-29)

   • Mambo yaliyofichwa, mambo yaliyofunuliwa (29)

 • 30

  • Kumrudia Yehova (1-10)

  • Amri za Yehova si ngumu sana (11-14)

  • Kuchagua kati ya uzima na kifo (15-20)

 • 31

  • Musa akaribia kufa (1-8)

  • Sheria yasomwa hadharani (9-13)

  • Yoshua awekwa kuwa kiongozi (14, 15)

  • Uasi wa Waisraeli watabiriwa (16-30)

   • Wimbo wa kuwafundisha Waisraeli (19, 22, 30)

 • 32

  • Wimbo wa Musa (1-47)

   • Yehova ni Mwamba (4)

   • Waisraeli wamsahau Mwamba wao (18)

   • “Kisasi ni changu” (35)

   • “Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake” (43)

  • Musa atafia juu ya Mlima Nebo (48-52)

 • 33

  • Musa ayabariki makabila (1-29)

   • ‘Mikono ya milele’ ya Yehova (27)

 • 34

  • Yehova amwonyesha Musa ile nchi (1-4)

  • Kifo cha Musa (5-12)