Mambo ya Walawi 15:1-33

15  Na Yehova akaendelea kusema na Musa na Haruni, na kuwaambia:  “Sema na wana wa Israeli, nanyi mtawaambia, ‘Ikiwa mwanamume yeyote ana mtiririko unaotoka+ katika kiungo chake cha uzazi, kile kinachomtoka si safi.  Nao huu utakuwa uchafu wake kutokana na kinachomtoka: Iwe kiungo chake cha uzazi kimetiririka kwa mtiririko unaotoka au kiungo chake cha uzazi kimezuiliwa kutokana na mtiririko wake unaotoka, huo ni uchafu wake.  “‘Kitanda chochote ambacho yule mwenye mtiririko unaotoka atalalia kitakuwa si safi, na chombo chochote ambacho atakalia kitakuwa si safi.  Na mtu ambaye atagusa kitanda chake atayafua mavazi yake, naye ataoga katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni.+  Na yeyote atakayeketi juu ya chombo chochote ambacho yule mwenye mtiririko unaotoka alikuwa amekalia atayafua+ mavazi yake, naye ataoga katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni.  Na yeyote atakayegusa mwili wa mtu mwenye mtiririko unaotoka+ atayafua mavazi yake, naye ataoga katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni.+  Na ikiwa mtu mwenye mtiririko unaotoka atamtemea mate mtu aliye safi, ndipo atayafua mavazi yake na kuoga katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni.  Na matandiko+ yoyote ambayo yule mwenye mtiririko unaotoka alikuwa ameyapanda yatakuwa si safi. 10  Na mtu yeyote atakayegusa chochote kilicho chini yake atakuwa asiye safi mpaka jioni; naye atakayevichukua atayafua mavazi yake, naye ataoga katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni. 11  Na mtu yeyote ambaye yule mwenye mtiririko unaotoka+ atamgusa kabla hajanawa mikono yake katika maji atayafua mavazi yake katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni. 12  Na chombo cha udongo ambacho yule mwenye mtiririko unaotoka atagusa kitavunjwa;+ na chombo chochote cha mbao+ kitaoshwa katika maji. 13  “‘Sasa, ikiwa yule mwenye mtiririko unaotoka atakuwa safi kutokana na mtiririko wake unaotoka, basi atajihesabia siku saba kwa ajili ya utakaso+ wake, naye atayafua mavazi yake na kuoga mwili wake katika maji yanayotiririka;+ naye atakuwa safi. 14  Na katika siku ya nane atajichukulia njiwa-tetere+ wawili au hua wawili wachanga, naye atakuja mbele za Yehova kwenye mwingilio wa hema la mkutano na kumpa kuhani. 15  Naye kuhani atawatoa, mmoja kuwa toleo la dhambi na yule mwingine kuwa toleo la kuteketezwa;+ naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Yehova kuhusiana na mtiririko wake unaotoka. 16  “‘Sasa, mwanamume akitokwa na shahawa,+ basi ataoga mwili wake wote katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni. 17  Na vazi lolote na ngozi yoyote ambazo shahawa iliyotoka itakuwa juu yake zitafuliwa katika maji nazo zitakuwa si safi mpaka jioni.+ 18  “‘Naye mwanamke ambaye mwanamume atalala naye na kutokwa na shahawa, wataoga katika maji na kuwa wasio safi+ mpaka jioni. 19  “‘Na ikiwa mwanamke ana mtiririko unaotoka, nao mtiririko wake unaotoka katika mwili wake uwe ni damu,+ ataendelea kwa siku saba kuwa katika uchafu+ wake wa hedhi,+ na yeyote atakayemgusa atakuwa asiye safi mpaka jioni. 20  Na kitu chochote ambacho atalalia katika uchafu wake wa hedhi kitakuwa si safi,+ na kila kitu ambacho atakalia kitakuwa si safi. 21  Na mtu yeyote anayegusa kitanda chake atayafua mavazi yake, naye ataoga katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni.+ 22  Na mtu yeyote atakayegusa chombo chochote alichokuwa akikalia atayafua mavazi yake, naye ataoga katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni.+ 23  Na ikiwa alikuwa amekalia kitanda au chombo kingine, kwa kukigusa+ atakuwa asiye safi mpaka jioni. 24  Na ikiwa mwanamume atalala naye na uchafu wake wa hedhi uwe juu yake,+ ndipo atakuwa asiye safi kwa siku saba, na kitanda chochote ambacho mwanamume huyo huenda akalalia kitakuwa si safi. 25  “‘Naye mwanamke, ikiwa mtiririko unaotoka wa damu yake utatiririka kwa siku nyingi+ wakati ambapo si wakati wa kawaida wa uchafu wake wa hedhi,+ au ikiwa atakuwa na mtiririko mrefu kuliko uchafu wake wa hedhi, siku zote za mtiririko wake unaotoka usio safi zitakuwa kama siku za uchafu wake wa hedhi. Yeye si safi. 26  Kitanda chochote ambacho huenda atalalia katika yoyote ya siku za mtiririko wake unaotoka kitakuwa kwake kitanda cha uchafu wa hedhi,+ na chombo chochote ambacho huenda atakalia kitakuwa si safi kama ule uchafu wake wa hedhi. 27  Na mtu yeyote atakayevigusa+ atakuwa asiye safi, naye atayafua mavazi yake na kuoga katika maji na kuwa asiye safi mpaka jioni. 28  “‘Hata hivyo, ikiwa amekuwa safi kutokana na mtiririko wake unaotoka, atajihesabia pia siku saba, kisha atakuwa safi.+ 29  Na katika siku ya nane atajichukulia njiwa-tetere+ wawili au hua wawili wachanga, naye atawaleta kwa kuhani katika mwingilio wa hema la mkutano.+ 30  Naye kuhani atamfanya mmoja kuwa toleo la dhambi na yule mwingine kuwa toleo la kuteketezwa;+ naye kuhani atafanya upatanisho+ kwa ajili yake mbele za Yehova kuhusiana na mtiririko wake unaotoka ambao si safi. 31  “‘Nanyi mtawatenga wana wa Israeli kutoka kwa uchafu wao, wasije wakafa katika uchafu wao kwa kuinajisi maskani yangu, iliyo katikati yao.+ 32  “‘Hiyo ndiyo sheria juu ya mwanamume aliye na mtiririko unaotoka+ na mwanamume ambaye ametokwa na shahawa+ na kuwa asiye safi kutokana nayo; 33  na mwanamke aliye na hedhi+ katika uchafu wake, na mtu yeyote aliye na mtiririko wake unaotoka,+ awe mwanamume au mwanamke, na awe ni mwanamume anayelala na mwanamke asiye safi.’”

Maelezo ya Chini