Kutoka 26:1-37

26  “Nayo maskani mtaifanya kwa vitambaa kumi vya mahema,+ kwa vitambaa vya kitani bora kilichosokotwa na uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili.+ Kwa makerubi,+ kazi ya mtarizi, utavifanya.  Urefu wa kila kitambaa cha hema utakuwa mikono 28 na upana wa kila kitambaa utakuwa mikono 4. Vitambaa hivyo vyote vitakuwa na kipimo kimoja.+  Vitambaa vitano vitafanyiza mfuatano, kimoja kikiwa kimeunganishwa na kingine, na vitambaa vitano vitafanyiza mfuatano, kimoja kikiwa kimeunganishwa na kingine.+  Nawe utafanya vitanzi vya uzi wa bluu kwenye upindo wa kile kitambaa kimoja kilicho mwisho wa mfuatano; nawe utafanya vivyo hivyo kwenye upindo wa kitambaa cha nje kabisa kilicho mahali pale pengine pa kuungania.+  Utafanya vitanzi 50 kwenye kitambaa kimoja, na vitanzi 50 utavifanya kwenye mwisho wa kitambaa kilicho mahali pale pengine pa kuungania, vitanzi vikikabiliana.+  Nawe utafanya kulabu 50 za dhahabu na kuviunganisha vitambaa hivyo, kimoja kwa kingine, kwa kulabu hizo, navyo vitakuwa maskani moja.+  “Nawe utafanya nguo za manyoya ya mbuzi+ kwa ajili ya hema juu ya maskani. Utafanya vitambaa kumi na moja vya mahema.  Urefu wa kila kitambaa utakuwa mikono+ 30, na upana wa kila kitambaa utakuwa mikono 4. Vitambaa vyote 11 vitakuwa na kipimo kimoja.  Nawe utaviunganisha vitambaa vitano pamoja, na vitambaa sita pamoja,+ nawe utakikunja mara mbili kile kitambaa cha sita kilicho upande wa mbele wa hema. 10  Nawe utafanya vitanzi 50 kwenye upindo wa kile kitambaa kimoja, cha nje kabisa kwenye ule mfuatano, na vitanzi 50 kwenye upindo wa kitambaa kilicho mahali pale pengine pa kuungania. 11  Nawe utafanya kulabu 50 za shaba+ na kuzitia kulabu hizo kwenye vile vitanzi na kuliunganisha lile hema pamoja, nalo litakuwa kitu kimoja.+ 12  Nacho kitambaa kitakachobaki kitakuwa cha kuning’inia. Nusu ya kitambaa cha hema kitakachobaki kitaning’inia upande wa nyuma wa maskani. 13  Na mkono mmoja wa upande huu na mkono mmoja wa upande ule wa kile kinachobakia katika urefu wa vitambaa utakuwa wa kuning’inia pande za maskani, ili kuifunika upande huu na upande ule. 14  “Nawe utafanya kifuniko cha hilo hema, kifuniko cha ngozi za kondoo-dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko cha ngozi za sili upande wa juu. 15  “Nawe utafanya viunzi+ vya mbao za mshita kwa ajili ya maskani hiyo, vinavyosimama mwishoni. 16  Urefu wa kiunzi utakuwa mikono kumi, nao upana wa kila kiunzi utakuwa mkono mmoja na nusu. 17  Kila kiunzi kitakuwa na ndimi mbili zilizounganishwa pamoja. Hivyo ndivyo utakavyofanya na viunzi vyote vya maskani. 18  Nawe utavifanya viunzi vya mbao kwa ajili ya maskani, viunzi 20 kwa ajili ya upande unaokabili Negebu, upande wa kusini. 19  “Nawe utafanya vikalio+ 40 vya fedha chini ya vile viunzi 20; vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja pamoja na ndimi zake mbili, na vikalio viwili chini ya kile kiunzi kingine pamoja na ndimi zake mbili. 20  Na kwa ajili ya upande ule mwingine wa maskani, upande wa kaskazini, viunzi 20,+ 21  na vikalio vyake 40 vya fedha, vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja na vikalio vingine viwili chini ya kile kiunzi kingine.+ 22  Na kwa ajili ya sehemu za nyuma za maskani kuelekea upande wa magharibi utafanya viunzi sita.+ 23  Nawe utafanya viunzi viwili viwe miimo ya pembeni ya maskani+ katika sehemu zake mbili za nyuma. 24  Navyo vitakuwa pacha sehemu ya chini, navyo vitakuwa pacha mpaka juu ya kila moja kwenye pete ya kwanza. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa ajili ya vyote viwili. Vitakuwa miimo miwili ya pembeni. 25  Na kutakuwa na viunzi vinane na vikalio vyake vya fedha, vikalio kumi na sita, vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja na vikalio viwili chini ya kile kiunzi kingine. 26  “Nawe utafanya miti ya mshita,+ mitano kwa ajili ya viunzi vya mbao vya upande mmoja wa maskani, 27  na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya upande ule mwingine wa maskani na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya upande wa maskani kwa ajili ya zile pande mbili za nyuma kuelekea upande wa magharibi.+ 28  Nao mti wa katikati ulio katikati ya viunzi utatoka mwisho mmoja mpaka mwingine. 29  “Nawe utavifunika vile viunzi vya mbao kwa dhahabu,+ na pete zake utazifanya kwa dhahabu ili zitegemeze ile miti; nawe utaifunika miti hiyo kwa dhahabu. 30  Nawe utaisimamisha maskani kulingana na ramani yake ambayo umeonyeshwa mlimani.+ 31  “Nawe utafanya pazia+ la uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa. Atalifanya likiwa na makerubi,+ kazi ya mtarizi. 32  Nawe utaliweka juu ya nguzo nne za mshita zilizofunikwa kwa dhahabu. Misumari yake itakuwa ya dhahabu. Zinakaa juu ya vikalio vinne vya fedha. 33  Nawe utaliweka pazia chini ya kulabu na kulileta sanduku la ushuhuda+ ndani ya hilo pazia; nalo pazia litawatenganishia Patakatifu+ na Patakatifu Zaidi.+ 34  Nawe utakiweka kifuniko juu ya sanduku la ushuhuda katika Patakatifu Zaidi. 35  “Nawe utaiweka meza nje ya pazia, na kinara cha taa+ kitakuwa upande tofauti na hiyo meza, kitakuwa upande wa maskani kuelekea kusini; nayo meza utaiweka upande wa kaskazini. 36  Nawe utafanya kisitiri+ kwa ajili ya mlango wa hema, kisitiri cha uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani safi kilichosokotwa, kazi ya mfumaji. 37  Nawe utakifanyizia kile kisitiri nguzo tano za mshita na kuzifunika kwa dhahabu. Vibanio vyake vitakuwa vya dhahabu. Nawe utavitengenezea vikalio vitano vya shaba.

Maelezo ya Chini