Hamia kwenye habari

Je, Yesu Alikuwa Mtu Mzuri tu?

Je, Yesu Alikuwa Mtu Mzuri tu?

Jibu la Biblia

Yesu hakuwa mtu mzuri tu. Jambo moja la hakika ni kwamba amethibitika kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa zaidi katika historia ya wanadamu. Ona mambo ambayo wanahistoria hawa na waandishi maarufu wamesema kumhusu:

“Yesu wa Nazareti . . . bila shaka ndiye mtu mashuhuri zaidi katika historia.”—H. G. Wells, mwanahistoria Mwingereza.

“Maisha [ya Yesu] yamekuwa na uvutano mkubwa zaidi katika sayari hii na uvutano wake unazidi kuongezeka.”—Kenneth Scott Latourette, mwanahistoria na mwandishi Mmarekani.

Biblia inaonyesha ni kwa nini Yesu amekuwa na ushawishi mkubwa zaidi kuliko mtu mwingine yeyote mzuri ambaye amewahi kuishi. Yesu alipowauliza wafuasi wake wa karibu zaidi walifikiri yeye ni nani, mmoja wao alijibu hivi kwa usahihi: “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”—Mathayo 16:16.