Hamia kwenye habari

Ufalme wa Mungu Utatimiza Nini?

Ufalme wa Mungu Utatimiza Nini?

Jibu la Biblia

 Ufalme wa Mungu utaondoa serikali zote za wanadamu na kuitawala dunia yote. (Danieli 2:44) Baada ya kutimiza hilo, Ufalme wa Mungu . . .

  •   Utawaondoa waovu, ambao wanatudhuru kwa sababu ya ubinafsi wao. “Nao waovu, watakatiliwa mbali kutoka duniani.”—Methali 2:22.

  •   Utakomesha vita vyote. “[Mungu] anakomesha vita mpaka kwenye mwisho wa dunia.”—Zaburi 46:9.

  •   Utaondoa umaskini na kuleta amani duniani. “Kila mtu ataishi kwa amani chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, na hakuna mtu atakayewaogopesha.”—Mika 4:4, Good News Translation.

  •   Utaigeuza dunia kuwa paradiso. “Majangwa yasiyokuwa na maji yatafurahi; mashamba yasiyozaa yatashangilia na kuchanua maua.”—Isaya 35:1, Contemporary English Version.

  •   Utaandaa kazi nzuri na yenye kufurahisha kwa kila mtu. “Watu [wa Mungu] waliochaguliwa wataitumia kazi ya mikono yao wenyewe kikamilifu. Hawatafanya kazi ya bure.”—Isaya 65:21-23.

  •   Utaondoa magonjwa. “Hakuna mkaaji atakayesema: ‘Mimi ni mgonjwa.’”—Isaya 33:24.

  •   Utatuondolea uzee. “Nyama yake na iwe laini kuliko wakati wa ujana; na arudi kwenye siku za nguvu za ujana wake.”—Ayubu 33:25.

  •   Utawafufua wafu. “Wote waliomo ndani ya makaburi ya ukumbusho wataisikia sauti yake [Yesu] na kutoka.”—Yohana 5:28, 29.