Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Je, Misiba ya Asili ni Adhabu Kutoka Kwa Mungu?

Je, Misiba ya Asili ni Adhabu Kutoka Kwa Mungu?

Jibu la Biblia

Biblia haifundishi kwamba Mungu ndiye anayesababisha misiba ya asili tunayoiona leo. Hukumu za Mungu zinazosimuliwa katika Biblia ni tofauti sana na misiba ya asili.

  1. Mungu huchagua mambo. Biblia inasema: “Mwanadamu huona kile kinachoonekana kwa macho, lakini Yehova huona jinsi moyo ulivyo.”—1 Samweli 16:7.

  2. Yehova husoma moyo wa mtu mmoja mmoja na kuwaharibu wale tu anaoona kuwa waovu.—Mwanzo18:23-32.

  3. Yehova hutoa onyo kwanza na hivyo kuwapa waadilifu fursa ya kuponyoka.

Kwa upande mwingine misiba ya asili hutokea bila onyo au baada ya kutoa dalili chache tu na huua na kuwaumiza watu bila kubagua. Kwa kiwango fulani, wanadamu wamefanya misiba hiyo kuwa mibaya zaidi kwa kuharibu mazingira na kujenga katika maeneo ambayo matetemeko ya nchi, mafuriko, na hali mbaya ya hewa hutokea mara nyingi.