Adamu na Hawa hawakumtii Mungu, basi wakafa. Mwanzo 3:6, 23

Hawa alimsikiliza nyoka na akala tunda lililokatazwa. Baadaye, alimpa Adamu, naye akala.

Kwa kufanya hivyo, walifanya dhambi ya kutotii. Mungu akawaondoa katika makao yao ya Paradiso.

Maisha yakawa magumu kwao na kwa watoto wao. Wakazeeka na kufa. Hawakwenda katika ulimwengu wa roho; walikoma kuwapo.

 Wafu hawana uhai kama vile mavumbi yasivyo na uhai. Mwanzo 3:19

Tunakufa kwa sababu sote ni wazao wa Adamu na Hawa. Wafu hawawezi kuona au kusikia au kufanya jambo lolote.—Mhubiri 9:5, 10.

Yehova hakukusudia watu wafe. Hivi karibuni, atawafufua wale wanaolala katika kifo. Iwapo watamsikiliza, wataishi milele.