Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Ni Nani Wanaofanya Mapenzi ya Yehova Leo?

 Somo la 23

Jinsi Machapisho Yetu Yanavyoandikwa na Kutafsiriwa

Jinsi Machapisho Yetu Yanavyoandikwa na Kutafsiriwa

Idara ya Uandikaji, Marekani

Korea Kusini

Armenia

Burundi

Sri Lanka

Ili tufanikiwe kutangaza “habari njema” katika “kila taifa na kabila na lugha na watu,” tunachapisha vitabu na magazeti katika lugha zaidi ya 700. (Ufunuo 14:6). Kazi hiyo yote inafanywaje? Tuna waandishi katika nchi mbalimbali na vilevile watafsiri wapatao 3,300. Wote hao ni Mashahidi wa Yehova.

Makala ya kwanza huandikwa katika Kiingereza. Baraza Linaloongoza husimamia kazi ya Halmashauri ya Uandikaji katika makao yetu makuu. Halmashauri hii huratibu kazi za waandikaji wanaoishi katika makao makuu na pia wale walio katika baadhi ya ofisi za tawi. Kwa sababu Halmashauri ya Uandikaji inatumia waandikaji wa nchi mbalimbali, machapisho yetu huwapendeza watu wa mataifa yote.

Makala hutumwa kwa watafsiri. Baada ya kuandikwa na kuidhinishwa, makala hutumwa kwa vikundi vya watafsiri kote duniani. Watafsiri hao hujitahidi kuchagua “maneno sahihi ya kweli” yanayotafsiri maana kamili katika lugha yao.—Mhubiri 12:10.

Kompyuta huharakisha kazi. Kompyuta haiwezi kufanya kazi zinazofanywa na waandikaji na watafsiri. Hata hivyo, kazi hiyo inaweza kuharakishwa kwa kutumia kamusi zilizo kwenye kompyuta, pamoja na vifaa vingine vya kufanyia utafiti. Mashahidi wa Yehova walibuni mfumo unaoitwa Multilanguage Electronic Publishing System (MEPS). Mfumo huo unawezesha maandishi ya mamia ya lugha kuingizwa kwenye kompyuta, kuunganishwa pamoja na picha, na kutayarishwa kwa ajili ya kuchapwa.

Kwa nini tufanye kazi yote hiyo ya uchapishaji, hata katika lugha zinazozungumzwa na maelfu machache tu ya watu? Kwa sababu ni mapenzi ya Mungu kwamba “watu wa namna zote waokolewe na kupata ujuzi sahihi wa kweli.”—1 Timotheo 2:3, 4.

  • Machapisho yetu huandikwa jinsi gani?

  • Kwa nini tunatafsiri machapisho yetu katika lugha nyingi sana?

Pata Kujua Mengi Zaidi

KAZI YA UCHAPISHAJI

Muziki Unaoimbwa Katika Lugha Nyingi

Soma kuhusu matatizo ya pekee ya kutafsiri maneno ya nyimbo katika lugha nyingi.