Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Eneo la juu la Svaneti

 GEORGIA

Maelezo Mafupi Kuhusu Georgia

Maelezo Mafupi Kuhusu Georgia

Kuvuna zabibu huleta shangwe kubwa

Nchi Georgia inajulikana kwa safu ya milima na vilele vyenye theluji, vingine vikiwa na urefu wa mita zaidi ya 4,500. Nchi hiyo imegawanywa katika sehemu mbili kuu, sehemu ya mashariki na ya magharibi, kila moja ikiwa na maeneo kadhaa yenye hali ya hewa, tamaduni, muziki, dansi, na chakula cha aina yake.

Watu Wengi wa wakazi wapatao milioni 3.7 ni Wageorgia.

Dini Idadi kubwa ya watu ni Waothodoksi. Asilimia 10 hivi ni Waislamu.

Lugha Kigeorgia hakihusiani na lugha yoyote ya nchi jirani. Historia inaonyesha kwamba alfabeti za pekee za Kigeorgia zilibuniwa Kabla ya Wakati wa Kawaida.

 Kazi Watu wengi hujitegemeza kupitia ukulima. Hivi karibuni, utalii umechangia pakubwa katika ukuzi wa uchumi nchini Georgia.

Hali ya hewa Sehemu ya mashariki ya nchi hiyo huwa na hali nzuri ya hewa. Eneo la pwani la Bahari Nyeusi, lililo magharibi mwa Georgia, huwa na hali nzuri ya hewa, na matunda ya jamii ya machungwa hukua kwa wingi.

Kuvuna zabibu katika eneo la Kakheti

 Chakula Kwenye kila mlo wa Mgeorgia, lazima kuwe na mkate. Mkate wa kitamaduni huokwa katika jiko la udongo. Chakula cha kawaida huwa mchuzi mzito wenye vikolezo na viungo vilivyotolewa moja kwa moja kutoka shambani. Divai imetengenezwa nchini Georgia kwa muda mrefu. Katika utamaduni wao, divai huchachishwa na kuwekwa kwenye vyombo vikubwa vya udongo. Familia nyingi hukuza zabibu na kujitengenezea divai. Nchini Georgia, kuna aina 500 hivi za zabibu za kienyeji.

Kuoka mkate wa kitamaduni