Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia

Hadithi ya 110: Timotheo—Msaidizi Mpya wa Paulo

Hadithi ya 110: Timotheo—Msaidizi Mpya wa Paulo

KIJANA unayeona hapa pamoja na mtume Paulo ni Timotheo. Timotheo anakaa pamoja na jamaa yake Listra. Jina la mama yake ni Eunike na nyanya yake Loisi.

Hii ndiyo mara ya tatu ya Paulo kutembelea Listra. Mwaka mmoja uliotangulia, Paulo na Barnaba walifika huku mara ya kwanza katika safari ya kuhubiri. Na sasa Paulo amerudi tena huko akiwa na rafiki yake Sila.

Timotheo na Paulo

Unajua Paulo anamwambia Timotheo nini? ‘Ungependa kwenda pamoja na Sila na mimi?’ anauliza. ‘Ungeweza kutusaidia kuhubiri watu wa mbali.’

‘Ndiyo,’ Timotheo ajibu, ‘ningependa kwenda.’ Basi upesi baada ya hapo Timotheo aacha jamaa yake na kwenda pamoja na Paulo na Sila. Lakini kabla ya kujifunza juu ya safari yao, na tujifunze ambayo yamekuwa yakimpata Paulo. Imekuwa miaka 17 tangu Yesu alipomtokea akienda Damasko.

Adui fulani wanafanya mpango wa kumwua Paulo kwa sababu hawataki mafundisho juu ya Yesu. Lakini wanafuzni wanamsaidia Paulo aokoke. Wanamweka katika kikapu na kumtelemsha nje ya ukuta wa mji.

Baada ya hayo Paulo aenda Antiokia kuhubiri. Huko ndiko kwa mara ya kwanza, wafuasi wa Yesu wanaitwa Wakristo. Ndipo Paulo na Barnaba wanatumwa kutoka Antiokia waende katika safari ya kuhubiri nchi za mbali sana. Mji mmoja ambao wanatembelea ni Listra, nyumbani kwa Timotheo.

Baadaye, kama mwaka mmoja, Paulo anarudi Listra katika safari ya pili. Timotheo anapokwenda na Paulo na Sila, unajua wanakwenda wapi? Angalia ramani, tujifunze sehemu chache.

Kwanza, wanakwenda kwenye mji wa Ikonio, kisha mji wa pili wa Antiokia. Baada ya hapo wanasafiri kwenda Tro′a, kisha Filipi, Thesalonike na Beroya. Unaona Athene katika ramani? Paulo anahubiri huko. Kisha wanakaa mwaka mmoja na nusu wakihubiri Korintho. Mwishowe wanasimama kidogo katika Efeso. Kisha wanarudi Kaisaria kwa meli, na kusafiri kwenda juu Antiokia, ambako Paulo anakaa.

Hivyo Timotheo anasafiri mamia na mamia yya kilomita akimsaidia Paulo azihubiri “habari njema” na kuanza makundi mengi ya Kikristo. Utakapokuwa mkubwa, je! utakuwa mtumishi mwaminifu wa Mungu kama Timotheo?

Matendo 9:19-30; 11:19-26; sura za 13 mpaka 17; 18:1-22.

Ramani

1. Roma; 2. Melita; 3. Beroya; 4. Thesalonike; 5. Korintho; 6. Filipi; 7. Athene; 8. Krete; 9. Troa; 10. Efeso; 11. Mileto; 12. Kolosai; 13. Antiokia; 14. Ikonio; 15. Listra; 16. Kipro; 17. Antiokia; 18. Kaisaria; 19. Yopa; 20. Damasko; 21. Yerusalemu; 22. Bahari Kuu (ya Kati) (Mediterania)Maswali

  • Kijana unayemwona katika picha ni nani, anaishi wapi, na mamake na nyanya yake wanaitwa nani?
  • Timotheo anasema nini Paulo anapomwuliza kama angetaka kujiunga na Sila na Paulo kuwahubiria watu katika maeneo ya mbali?
  • Wafuasi wa Yesu wanaitwa Wakristo kwa mara ya kwanza wapi?
  • Baada ya kuondoka Antiokia, Paulo, Sila, na Timotheo wanatembelea miji gani?
  • Timotheo anamsaidiaje Paulo, na vijana wanapaswa kujiuliza maswali gani leo?

Maswali ya ziada