Siku ya tatu baada ya kufa kwake, Yesu alifufuliwa. Siku hiyo akaonekana kwa wafuasi wake mara tano zilizo tofauti. Yesu akaendelea kuonekana kwao kwa siku 40. Kisha, wengine kati ya wanafunzi wake walipokuwa wakitazama, Yesu akapanda mbinguni. Siku kumi baadaye Mungu alimwaga roho takatifu juu ya wafuasi wa Yesu waliokuwa wakingoja Yerusalemu.

Baadaye, adui za Mungu wakasababisha kufungwa kwa mitume gerezani, lakini malaika aliwafungua. Wapinzani walimpiga mwanafunzi Stefano kwa mawe akafa. Lakini twajifunza jinsi Yesu alivyomchagua mmoja wa wapinzani hao awe mtumishi wake wa pekee, akawa mtume Paulo. Ndipo, miaka mitatu na nusu baada ya kufa kwa Yesu, Mungu akamtuma mtume Petro akamhubiri Kornelio asiye Myahudi na jamaa yake.

Karibu miaka 13 baadaye Paulo alianza safari yake ya kuhubiri. Katika safari yake ya pili Timotheo ajiunga na Paulo. Twajifunza jinsi Paulo na wasafiri wenzake walivyoona mambo mengi ya kufurahisha katika kumtumikia Mungu. Mwishowe, Paulo akafungwa Roma. Miaka miwili baadaye akafunguliwa, lakini akafungwa tena na kuuawa. Matukio ya SEHEMU ya 7 yalitukia kwa muda wa miaka kama 32.

Sauli awa kipofu kwa sababu ya nuru