TURUDI kwenye miaka michache kabla Ezra hajaenda Yerusalemu. Mordekai na Esta (Esiteri) ni Waisraeli wenye vyeo vya juu katika ufalme wa Ajemi. Esta ndiye malkia, na Mordekai binamu yake ni wa pili kwa mfalme katika mamlaka. Na tuone hayo yalivyotokea.

Wazazi wa Esta walikufa wakati alipokuwa mtoto mdogo sana, Mordekai akamlea. A·has·ue′ro, mfalme wa Ajemi, ana jumba la kifalme mjini Shu′shani, naye Mordekai ni mmoja wa watumishi wake. Basi, siku moja Vash′ti mke wa mfalme anakataa kumtii, hivyo mfalme anachagua mke mwingine awe malkia wake. Unajua anachagua mwanamke gani? Esta msichana mrembo.

Hamani mwenye ghadhabu pamoja na Mordekai

Wamwona mtu huyu mwenye kiburi anayeinamiwa na watu? Ni Hamani. Ana cheo cha juu katika Ajemi. Hamani anataka Mordekai, unayeona ameketi hapa, amwinamie pia. Lakini Mordekai anakataa. Haoni yafaa kumwinamia mtu huyo mbaya. Hiko linamkasirisha sana Hamani. Basi anafanya hivi.

Hamani anamwambia mfalme uongo juu ya Waisraeli. “Ni watu wabaya wasiotii sheria zako,’ asema. ‘Wanapaswa kuuawa.’ A·has·ue′ro hana habari kwamba Esta mkewe ni Mwisraeli. Basi amsikiliza Hamani, na kuogiza sheria itungwe Waisraeli wauawe siku fulani.

Mordekai anapopata habari ya sheria hiyo, anaona vibaya sana. Anampelekea Esta ujumbe huu: ‘Lazima umwambie mfalme, na kumwomba atuokoe.’ Ni kinyume cha sheria katika Ajemi kumwona mfalme bila kuitwa. Lakini Esta aingia bila kuitwa. Mfalme amnyoshea fimbo yake ya dhahabu, maana yake asiuawe. Esta anamwalika mfalme na Hamani kwenye karamu. Wakiwa huko mfalme amwuliza Esta anachotaka mfalme ampe. Esta asema atamwambia ikiwa yeye na Hamani watakuja kwenye karamu nyingine kesho yake.

Katika karamu hiyo Esta amwambia mfalme hivi: ‘Watu wangu na mimi tutauawa.’ Mfalme anakasirika. ‘Nani anathubutu kufanya hivyo?’ auliza.

‘Mtu huyo, adui huyo, ndiye huyu Hamani mbaya!’ Esta asema.

Malkia Esta akimshtaki Hamani

Sasa mfalme akasirika kweli kweli. Anaamuru Hamani auawe. Kisha, mfalme anampa Mordekai cheo cha pili katika mamlaka. Ndipo Mordekai anahakikisha sheria mpya itungwe kuruhusu Waisraeli wapiganie uhai wao siku ambayo wangeuawa. Kwa kuwa sasa Mordekai ana cheo, watu wengi wanasaidia Waisraeli, nao wanaokolewa na adui zao.

Kitabu cha Biblia cha Esta (Esiteri).Maswali

  • Mordekai na Esta ni nani?
  • Kwa nini Mfalme Ahasuero anataka mke mpya, na anamchagua nani?
  • Hamani ni nani, na kwa nini amekasirika sana?
  • Ni sheria gani inayotungwa, na Esta anafanya nini baada ya kupata ujumbe kutoka kwa Mordekai?
  • Inakuwaje kwa Hamani na Mordekai?
  • Waisraeli wanaepukaje kuuawa na adui zao?

Maswali ya ziada