Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia

Hadithi ya 61: Daudi Anafanywa Mfalme

Hadithi ya 61: Daudi Anafanywa Mfalme

TENA Sauli anajaribu kumkamata Daudi. Anachukua askari wake bora zaidi 3,000 na kwenda kumtafuta. Daudi anapojua hivyo, anatuma wapelelezi ajue mahali ambapo Sauli na watu wake wamepiga kambi walale usiku. Ndipo Daudi anawaambia watu wake hivi: ‘Ni nani atakayekwenda pamoja nami kwenye kambi ya Sauli?’

Daudi akimwita Mfalme Sauli

‘Mimi,’ Abishai anajibu. Abishai ni mwana wa Seruya dada yake Daudi. Wakati Sauli na watu wake wamelala, Daudi na Abishai wanaingia kambini kimya-kimya. Wanachukua mkuki na mtungi wa Sauli, kando ya kichwa cha Sauli. Hakuna mtu anayeona wala kuwasikia kwa sababu wote wamelala sana.

Ebu mwone sasa Daudi na Abishai. Wamekwisha kwenda mbali, nao wako salama juu ya kilima. Daudi anampazia sauti mkuu wa jeshi la Israeli hivi: ‘We-e Abneri, sababu gani humlindi bwanako, mfalme? Tazama! Mkuki na mtungi wake viko wapi?’

Sauli anaamka. Aitambua sauti ya Daudi, kisha auliza: ‘Ni wewe, Daudi?’ Unaweza kumwona Sauli na Abneri chini kule?

‘Ndiyo, bwanangu mfalme,’ Daudi amjibu Sauli. Naye Daudi auliza hivi: ‘Kwa nini wataka kunikamata? Nimefanya ubaya gani? Mkuki wako huu, Ee mfalme. Mtume mmoja wa watu wako aje auchukue.’

Mfalme Sauli na Abneri

‘Nimekosa,’ Sauli anakubali. ‘Nimetenda kipumbavu.’ Ndipo Daudi anakwenda zake, naye Sauli anarudi kwake. Lakini Daudi anajisemesha hivi: ‘Siku fulani Sauli ataniua mimi. Yanipasa nikimbie niende kwenye nchi ya Wafilisti.’ Anafanya hivyo. Daudi anapumbaza Wafilisti na kuwafanya waamini yuko upande wao.

Wakati fulani baadaye Wafilisti wanakwenda kupigana na Israeli. Huko vitani, Sauli na Yonathani wanauawa. Hilo lamhuzunisha Daudi sana, naye anaandika wimbo mzuri, akiimba hivi: ‘Naona huzuni kwa ajili yako, ndugu yangu Yonathani. Jinsi nilivyokupenda!’

Baada ya hayo Daudi anarudi Israeli kenye mji wa Hebroni. Kwatokea vita kati ya watu wanaochagua Ishiboshethi mwana wa Sauli, awe mfalme, na watu wengine wanaotaka Daudi awe mfalme. Lakini mwishowe watu wa Daudi wanashinda. Sasa Daudi ni mwenye miaka 30 anapofanywa kuwa mfalme. Anatawala katika Hebroni kwa miaka saba na nusu.

Wakati wafika wa Daudi na watu wake kwenda kuteka mji mzuri unaoitwa Yerusalemu. Yoabu, mwana mwingine wa Seruya, dada yake Daudi, anaongoza vita. Basi Daudi anamfanya Yoabu kuwa mkuu wa jeshi lake. Sasa Daudi anaanza kutawala katika mji wa Yerusalemu.

1 Samweli 26:1-25; 27:1-7; 31:1-6; 2 Samweli 1:26; 3:1-21; 5:1-10; 1 Nyakati 11:1-9.Maswali

  • Daudi na Abishai walifanya nini Sauli alipolala usingizi kambini mwake?
  • Daudi anamwuliza Sauli maswali yapi?
  • Baada ya kumwacha Sauli, Daudi anakwenda wapi?
  • Ni nini kinachomhuzunisha Daudi sana, hivi kwamba anatunga wimbo mzuri?
  • Daudi ana umri gani anapowekwa kuwa mfalme huko Hebroni, na baadhi ya wanawe wanaitwa nani?
  • Daudi anatawala katika mji gani baadaye?

Maswali ya ziada