Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Hadithi ya 42: Punda Anasema

Hadithi ya 42: Punda Anasema

JE! UMEPATA kusikia kwamba punda anasema? ‘Hapana,’ labda unasema. ‘Wanyama hawawezi kusema.’ Lakini Biblia inasimulia hivyo. Na tuone ilivyokuwa.

Malaika

Waisraeli wako karibu sana kuingia nchi ya Kanaani. Balaki, mfalme wa Moabu, anawaogopa Waisraeli. Basi anapeleka habari ili mtu mwerevu jina lake Balaamu awalaani Waisraeli. Balaki anaahidi kumpa Balaamu fedha nyingi sana, basi Balaamu anapanda punda wake kwenda kumwona Balaki.

Yehova hataki Balaamu alaani watu wake. Basi anamtuma malaika mwenye upanga mrefu akasimame njiani amzuie Balaamu. Balaamu hawezi kumwona malaika, lakini punda anamwona. Basi punda huyo anaepa-epa huyo malaika, na mwishowe analala njiani. Balaamu anakasirika sana, na kumpiga punda wake kwa fimbo.

Ndipo Yehova anamfanya Balaamu asikie punda wake akisema naye. ‘Nimekukosea nini hata unipige?’ punda anauliza.

Balaamu akiwa amepanda punda

‘Umenifanya mpumbavu,’ Balaamu anasema. ‘Kama ningekuwa na upanga ningekuua!’

‘Je! nimekufanyia hivyo zamani?’ punda anauliza.

‘Hapana,’ Balaamu anajibu.

Ndipo Yehova anamwonyesha Balaamu malaika aliye na upanga anasimama njiani. Malaika anasema hivi: ‘Kwa nini umempiga punda wako? Nimekuja nikuzuie njia usiende kulaani Waisraeli. Kama punda wako hangeniepa, ningekupiga ufe.’

Balaamu anasema: ‘Nimefanya dhambi. Sikujua kama ulikuwa ukisimama njiani.’ Malaika huyo anamruhusu Balaamu aende, naye Balaamu anaendelea na safari ya kumwona Balaki. Bado anajaribu kulaani Waisraeli, lakini, badala yake, Yehova anamwongoza abariki Waisraeli mara tatu.

Hesabu 21:21-35; 22:1-40; 23:1-30; 24:1-25.Maswali

  • Balaki ni nani, na kwa nini anamwita Balaamu aje?
  • Kwa nini punda wa Balaamu amelala njiani?
  • Balaamu anamsikia punda akisema nini?
  • Malaika anamwambia Balaamu nini?
  • Inakuwaje Balaamu anapojaribu kuwalaani Waisraeli?

Maswali ya ziada