Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Hadithi ya 37: Hema ya Ibada

Hadithi ya 37: Hema ya Ibada

UNAJUA jengo hili? Ni hema ya pekee ya kuabudia Yehova. Watu walimaliza kuijenga mwaka mmoja baada ya kuondoka Misri. Unajua aliyetoa wazo la kuijenga?

Hema ya ibada

Ni Yehova. Musa alipokuwa katika Mlima Sinai, Yehova alimwambia namna ya kuijenga. Alimwambia ijengwe ili iwe vyepesi kubomolewa. Kwa njia hiyo sehemu zake zingeweza kuchukuliwa mahali pengine, na kuunganishwa tena. Basi Waisraeli walipokuwa wakihama hapa na pale jangwani, walichukua hema hiyo.

Ukitazama ndani ya chumba kidogo mwishoni mwa hema, unaweza kuona sanduku, au kasha. Hilo laitwa sanduku la agano. Kila upande ulikuwa na malaika au kerubi mmoja wa dhahabu. Tena Mungu aliziandika Amri Kumi juu ya mabamba mawili ya mawe, kwa sababu Musa alikuwa ameyavunja yale ya kwanza. Na mawe hayo yalitunzwa ndani ya sanduku la agano. Pia, mtungi wa mana ulitunzwa ndani yake. Unakumbuka mana ni nini?

Yehova anachagua Haruni ndugu yake Musa awe kuhani mkuu. Anawaongoza watu wamwabudu Yehova. Na wanawe ni makuhani pia.

Sasa kitazame chumba kikubwa zaidi cha hema hiyo. Ni kikubwa mara mbili kuliko kile chumba kidogo. Unaliona lile sanduku au kasha dogo, na moshi kidogo ukipanda kutoka ndani yake? Ndiyo madhabahu ambapo makuhani wanachoma uvumba. Halafu kuna kinara cha taa chenye taa saba. Na kitu cha tatu chumbani ni meza. Mikate 12 inatunzwa juu yake.

Uani mwa hema mna bakuli kubwa, au birika, iliyojaa maji. Makuhani wanaitumia kwa kuogea. Pia kuna madhabahu kubwa. Hapo ndipo wanyama wafu wanapochomwa wawe toleo kwa Yehova. Hema iko katikati ya kambi, na Waisraeli wanakaa katika hema zao kuizunguka.

Kutoka 25:8-40; 26:1-37; 27:1-8; 28:1; 30:1-10, 17-21; 34:1, 2; Waebrania 9:1-5.Maswali

  • Ni jengo gani unaloona katika picha, na ni la nini?
  • Kwa nini Yehova alimwambia Musa hema lijengwe kwa njia ambayo lingeweza kubomolewa kwa urahisi?
  • Ni sanduku gani lililo katika chumba kidogo kwenye sehemu ya mwisho ya hema, na kuna nini ndani ya sanduku hilo?
  • Yehova anamchagua nani kuwa kuhani mkuu, na kuhani mkuu anafanya kazi gani?
  • Taja vile vitu vitatu vilivyo katika chumba kikubwa hemani.
  • Ni vitu gani viwili vilivyo kwenye ua wa hema, navyo hutumiwa kwa njia gani?

Maswali ya ziada