Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia

Sehemu 3: Kukombolewa Misri Mpaka Mfalme wa Kwanza wa Israeli

Sehemu 3: Kukombolewa Misri Mpaka Mfalme wa Kwanza wa Israeli

Musa aliwaongoza Waisraeli kutoka utumwa wa Misri kwenda kwenye Mlima Sinai, ambako Mungu aliwapa sheria zake. Baadaye, Musa akawatuma wanaume 12 wakapeleleze nchi ya Kanaani. Lakini 10 kati yao wakarudisha ripoti mbaya. Waliwafanya watu watake kurudi Misri. Kwa kukosa imani, Mungu aliwaadhibu Waisraeli kwa kuwafanya watange-tange jangwani muda wa miaka 40.

Mwishowe, Yoshua akachaguliwa aongoze Waisraeli kuingia nchi ya Kanaani. Ili kuwasaidia waichukue nchi hiyo Yehova alifanya miujiza mingi. Alifanya maji ya Mto Yordani yaache kutiririka, kuta za Yeriko zianguke, jua lisimame bila kwenda kwa siku nzima. Baada ya miaka sita, nchi hiyo ikachukuliwa kutoka kwa Wakanaani.

Kuanzia na Yoshua, Waisraeli walitawalwa na mahakimu (waamuzi) muda wa miaka 356. Twajifunza habari za wengi wao, kutia Baraki, Gideoni, Yeftha, Samsoni na Samweli. Pia twasoma habari za wanawake kama Rahabu, Debora, Yaeli, Ruthu, Naomi na Delila. Kwa jumla, Sehemu ya 3 inasimulia historia ya miaka 396.

Hema la kukutania