YUSUFU ana miaka 17 tu anapopelekwa Misri. Anauzwa kwa Potifa. Potifa anafanya kazi ya mfalme wa Misri, anayeitwa Farao.

Yusufu akiwa gerezani

Yusufu anafanya kazi ya bwana wake, Potifa, kwa bidii. Kwa nini Yusufu amewekwa humu ndani ya gereza? Ni kwa sababu ya mke wa Potifa.

Yusufu anakuwa mwanamume mwenye sura nzuri sana, mke wa Potifa anataka alale naye. Lakini Yusufu anajua hilo ni kosa, hawezi kulifanya. Mke wa Potifa anakasirika sana. Basi mume anaporudi nyumbani, anamwambia uongo na kusema: ‘Yusufu huyo mbaya alitaka kulala nami!’ Potifa anamwamini mke wake, naye anamkasirikia sana Yusufu. Basi anamtupa gerezani.

Upesi msimamizi wa gereza aona Yusufu ni mtu mzuri. Basi anamweka kuwa msimamizi wa wafungwa wengine wote. Baadaye Farao akamkasirikia mnyweshaji wake na mwokaji wake, na kuwatia gerezani. Usiku mmoja kila mmoja wao anaota ndoto ya pekee, lakini hawajui maana ya ndoto zao, kesho yake Yusufu anasema: ‘Niambieni ndoto zenu.’ Wanamwambia. Na kwa msaada wa Mungu, Yusufu anawaambia maana ya ndoto zao.

Kwa mnyweshaji, Yusufu anasema: Kwa siku tatu utafunguliwa utoke gerezani , uwe mnyweshaji wa Farao tena.’ Lakini kwa mwokaji, Yusufu anasema: ‘Katika siku tatu Farao atakukata kichwa chako.’

Katika muda wa siku tatu inakuwa kama Yusufu alivyosema. Farao anamkata kichwa mwokaji wake. Lakini mnyweshaji, anafunguliwa gerezani na kuanza kumtumikia mfalme tena. Lakini mnyweshaji huyo anamsahau Yusufu! Hamwambii Farao habari zake, naye Yusufu anaendelea kukaa gerezani.

Mwanzo 39:1-23; 40:1-23.Maswali

  • Yusufu ana umri gani anapopelekwa Misri, na ni jambo gani linalotukia anapofika huko?
  • Kwa nini Yusufu anafungwa gerezani?
  • Yusufu anapewa daraka gani gerezani?
  • Anapokuwa gerezani Yusufu anamsaidiaje mnyweshaji na mwokaji wa Farao?
  • Ni jambo gani linalotukia baada ya mnyeshwaji kuachiliwa kutoka gerezani?

Maswali ya ziada