Watu wanane peke yao ndio waliookoka Gharika, lakini baadaye wakaongezeka kuwa maelfu mengi. Kisha, ilipopita miaka 352 baada ya Gharika, Abrahamu akazaliwa. Tunajifuzna namna Mungu alivyotimiza ahadi yake kwa kumpa Abrahamu mwana anayeitwa Isaka. Kisha, kati ya wana wawili wa Isaka, Yakobo alichaguliwa na Mungu.

Yakobo alikuwa na jamaa kubwa ya wana 12 na binti fulani. Wana 10 wa Yakobo walimchukia ndugu yao mdogo Yusufu wakamwuza utumwani huko misri. Baadaye, Yusufu akawa mtawala mkuu wa Misri. Njaa kuu ilipotokea, Yusufu aliwajaribu ndugu zake aone kama wamegeuza moyo. Halafu, jamaa yote ya Yakobo, yaani, Waisraeli, wakahamia Misri. Hayo yalitokea miaka 290 baada ya kuzaliwa Abrahamu.

Kwa miaka 215 iliyofuata Waisraeli walikaa huko Misri. Yusufu alipokufa, wakawa watumwa huko. Mwishowe, Musa akazaliwa, naye Mungu akamtumia awakomboe Waisraeli kutoka Misri. Kwa jumla, miaka 857 ya historia inazungumzwa katika Sehemu ya 2.

Familia ya inahamia Misri