Watu wakimcheka Nuhu

NUHU alikuwa na mke na wana watatu. Wana hao ni Shemu, Hamu na Yafeti. Kila mmoja wao alikuwa na mke. Kwa hiyo, jamaa ya Nuhu ilikuwa yenye watu nane.

Mungu akamwagiza Nuhu afanye jambo geni. Alimwambia ajenge safina kubwa. Safina hiyo ilikuwa kubwa kama meli, lakini ilionekana kama sanduku kubwa, refu. ‘Fanya iwe urefu wa vyumba vitatu kwenda juu,’ Mungu akasema, ‘uweke vyumba ndani yake.’ Vyumba hivyo vilikuwa vya Nuhu na jamaa yake, wanyama, na chakula chao.

Tena Mungu akamwambia Nuhu aikaze safina hiyo ili maji yasiweze kuingia. Mungu akasema: ‘Nitaleta gharika kubwa iharibu ulimwengu mzima. Kila mtu nje ya safina atakufa.

Nuhu na wanawe walimtii Yehova wakaanza kujenga safina. Lakini watu wengine walikuwa wakicheka tu. Walizidi kuwa wabaya.

Familia ya Nuhu ikiingiza wanyama na chakula ndani ya safina

Kujenga safina kulichukua muda mrefu kwa sababu ilikuwa kubwa mno. Baada ya miaka mingi, ikamalizika. Kisha Mungu akamwambia Nuhu aingize wanyama katika safina. Tena Mungu alimwambia Nuhu aingize namna zote mbalimbali za ndege. Nuhu akafanya kama Mungu alivyosema.

Kisha, Nuhu na jamaa yake wakaingia katika safina. Ndipo Mungu akaufunga mlango. Nuhu na jamaa yake walingoja humo ndani. Je! kweli gharika ingekuja kama vile Mungu alivyosema?

Mwanzo 6:9-22; 7:1-9.Maswali

  • Familia ya Nuhu ilikuwa na watu wangapi, na wanawe watatu waliitwa nani?
  • Mungu alimwagiza Nuhu afanye jambo gani lisilo la kawaida, na kwa nini?
  • Majirani wa Nuhu walifanya nini alipowaambia kuhusu safina?
  • Mungu alimwambia Nuhu afanye nini na wanyama?
  • Baada ya Mungu kufunga mlango wa safina, ilimbidi Nuhu na familia yake kufanya nini?

Maswali ya ziada