TAZAMA yanayotendeka sasa. Adamu na Hawa wanafukuzwa katika bustani nzuri ya Edeni. Unajua sababu?

Adamu na Hawa wanafukuzwa katika bustani ya Edeni

Walifanya jambo baya sana. Yehova anawaadhibu. Unajua jambo baya ambalo Adamu na Hawa walifanya?

Ni jambo ambalo Mungu aliwakataza. Mungu aliwaambia wale chakula cha miti ya bustani. Lakini si cha mti ambao Mungu aliwakataza, ili wasife. Huo ulikuwa mti wake peke yake. Tunajua ni makosa kuchukua kitu cha mtu mwingine, sivyo? Basi, kulitokea nini?

Siku moja Hawa alipokuwa peke yake katika bustani, nyoka alisema naye. Ajabu! Akamwambia Hawa ale tunda la mti ambao Mungu aliwakataza. Yehova hakuumba nyoka waseme. Mtu fulani alifanya nyoka aseme. Ni nani?

Si Adamu. Ni mmoja wa watu ambao Yehova alikuwa ameumba zamani kabla ya dunia. Ni malaika ambao hatuwezi kuona. Malaika huyo mmoja akawa na kiburi sana. Alianza kuwaza kwamba ingefaa atawale kama Mungu. Alitaka watu wamtii yeye kuliko Yehova. Huyo ndiye malaika aliyemfanya nyoka aseme.

Malaika huyo alimdanganya Hawa. Alipomwambia watafanana na Mungu wakila tunda hilo, Hawa aliamini. Hawa akala, hata Adamu. Adamu na Hawa hawakumtii Mungu. Ndiyo sababu walipoteza makao yao mazuri.

Lakini siku moja Mungu ataifanya dunia nzima iwe nzuri kama bustani ya Edeni. Tutajifunza namna wewe unaweza kushiriki kuifanya hivyo. Lakini sasa, tuchunguze yaliyowapata Adamu na Hawa.

Mwanzo 2:16, 17; 3:1-13, 24; Ufunuo 12:9.Maswali

  • Ni nini kinachowapata Adamu na Hawa kama unavyoona katika picha hii?
  • Kwa nini Yehova aliwaadhibu?
  • Nyoka alimwambia Hawa nini?
  • Ni nani aliyemfanya nyoka aseme na Hawa?
  • Kwa nini Adamu na Hawa hawakuruhusiwa kuendelea kuishi katika Paradiso?

Maswali ya ziada