Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia

Hadithi ya 3: Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza

Hadithi ya 3: Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza

UNAONA tofauti gani katika picha hii? Kuna watu. Mwanamume na mwanamke wa kwanza. Nani aliwaumba? Ni Mungu. Unajua jina lake? Ni Yehova. Mwanamume na mwanamke waliitwa Adamu na Hawa.

Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni

Yehova Mungu aliumba Adamu hivi. Alichukua mavumbi akafanya mwili mzuri wa mwanamume. Kisha akapuliza katika pua, Adamu akawa hai.

Yehova Mungu alimpa Adamu kazi ya kuwapa wanyama wote majina. Labda Adamu aliwatazama wanyama muda mrefu ili aweze kuwachagulia wote majina bora. Adamu alipokuwa akiwapa wanyama majina, aliona jambo fulani. Unajua ni jambo gani?

Wanyama wote walikuwa na wenzao. Tembo baba na mama walikuwapo, hata simba baba na mama. Lakini Adamu hakuwa na mwenzake. Basi Yehova akampa Adamu usingizi mzito, akachukua ubavu wake mmoja. Kwa ubavu huo, Yehova alimfanyia Adamu mke.

Adamu akafurahi! Wazia Hawa alivyofurahi alipowekwa katika bustani hiyo nzuri! Wangeweza kuzaa watoto wakae pamoja kwa furaha.

Yehova alitaka Adamu na Hawa wakae milele. Alitaka waifanye dunia nzima iwe nzuri kama bustani hii ya Edeni. Adamu na Hawa walifurahia sana hilo! Wewe ungependa kuifanya dunia iwe bustani nzuri? Lakini furaha ya Adamu na Hawa haikuendelea. Na tuone kwa nini.

Zaburi 83:18; Mwanzo 1:26-31; 2:7-25.Maswali

  • Kuna tofauti gani kati ya picha ya Hadithi ya 3 ni tofauti na picha ya Hadithi ya 2?
  • Ni nani aliyemwumba mtu wa kwanza, na mtu huyo aliitwa nani?
  • Mungu alimpa Adamu kazi gani ya kufanya?
  • Kwa nini Mungu alimfanya Adamu alale usingizi mzito?
  • Adamu na Hawa wangaliweza kuishi kwa muda gani, na Yehova alitaka wafanye kazi gani?

Maswali ya ziada