Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Hadithi ya 1: Mungu Aanza Kuumba Vitu

Hadithi ya 1: Mungu Aanza Kuumba Vitu

VITU vizuri vyote tulivyo navyo vimetoka kwa Mungu. Aliumba jua litupe mwangaza mchana, mwezi na nyota usiku. Tena Mungu akaumba dunia tukae ndani yake.

Lakini kwanza Mungu hakuumba jua, mwezi, nyota na dunia. Unajua alivyoumba kwanza? Mungu aliumba watu walio kama yeye. Hatuwezi kuona watu hao, kama vile hatuwezi kumwona Mungu. Biblia inawaita watu hao malaika. Mungu aliumba malaika wakae na yeye mbinguni.

Malaika ambaye Mungu aliumba kwanza alikuwa wa pekee sana. Alikuwa Mwana wa kwanza wa Mungu, akafanya kazi pamoja na Baba yake. Alimsaidia Mungu kuumba vitu vingine vyote. Tena alimsaidia Mungu kuumba jua, mwezi, nyota na dunia yetu.

Wakati huo dunia ilikuwa namna gani? Mwanzoni mtu hangeweza kukaa duniani. Nchi yote ilikuwa bahari kubwa. Lakini Mungu alitaka watu wakae duniani Akaanza kutayarisha makao yetu. Alifanya nini?

Kwanza dunia ilitaka nuru. Basi Mungu akaifanya nuru ya jua iangazie dunia. Alifanya hivyo ili kuwe usiku na mchana. Kisha Mungu akatokeza nchi kavu juu ya maji ya bahari.

Kwanza nchi haikuwa na kitu. Ilikuwa kama picha unayoona hapa. Maua hayakuwapo, wala miti wala wanyama. Hata samaki hawakuwamo baharini. Mungu alikuwa na kazi zaidi ili dunia iwe makao yanayofaa sana ya wanyama na watu.

Yeremia 10:12; Wakolosai 1:15-17; Mwanzo 1:1-10.

Nchi tasa


Maswali

  • Vitu vyote vizuri vimetoka wapi, unaweza kutaja kitu kimoja kizuri?
  • Mungu alimwumba nani kwanza?
  • Kwa nini malaika wa kwanza alikuwa wa pekee?
  • Elezea jinsi dunia ilivyoonekana mwanzoni?
  • Mungu alifanya nini kwanza ili kutayarisha dunia kwa ajili ya wanyama na wanadamu?

Maswali ya ziada