MARA nyingi, matetemeko, tsunami, na milipuko ya volkano huathiri maisha ya watu nchini Indonesia. Majanga yanapotokea watu wa Yehova hufanya haraka kuwasaidia, hasa Wakristo wenzao. Kwa mfano, mwaka wa 2005, tetemeko kubwa lilikumba Gunungsitoli, mji mkubwa katika kisiwa cha Nias, Sumatra Kaskazini. Makutaniko ya kisiwa jirani cha Sumatra na ofisi ya tawi yalituma msaada haraka katika maeneo yaliyoathiriwa. Mwangalizi wa mzunguko wa eneo hilo na mwakilishi wa ofisi ya tawi walisafiri kwenda kuwatia moyo na kuwafariji akina ndugu. Yuniman Harefa mzee wa Nias anasema hivi:“Watu walijawa na hofu. Hata hivyo, msaada kutoka Tengenezo la Mungu ulituhakikishia kwamba hatuko peke yetu.