• ALIZALIWA 1963

  • ALIBATIZWA 1995

  • HISTORIA FUPI Mzee aliyechunga kundi kwa upendo wakati wa mgogoro wa kidini huko Ambon, ambacho ni sehemu ya Visiwa vya Maluku.

MNAMO Januari 19, 1999, mgogoro uliongezeka kati ya Waislamu na Wakristo na ulisababisha vurugu kubwa kilomita tatu kutoka nyumbani kwangu. Hali ilikuwa mbaya sana. *

Baada ya kuhakikisha kwamba familia yangu iko salama, niliwapigia simu wahubiri wengine ili kujua hali zao. Niliwasihi watulie na wasiende kwenye maeneo hatari. Baadaye, wazee waliwatembelea ili kuwaimarisha kiroho na kuwatia moyo wafanye mikutano katika vikundi vidogo.

Ofisi ya tawi ilipendekeza kwamba wahubiri wote wanaoishi katika maeneo hatari waondoke, hivyo tukazijulisha familia kadhaa kuhusiana na mwongozo huo. Ndugu mmoja aliyepuuza maagizo hayo aliuawa na kundi la wahalifu. Hata hivyo, waliofuata mwongozo wa ofisi ya tawi waliokoka.

^ fu. 1 Mgogoro huo ulienea katika jimbo lote la Maluku kwa zaidi ya miaka miwili na maelfu ya watu walikimbia nyumba zao.