Nchi Theluthi mbili za kisiwa cha Hispaniola ni Jamhuri ya Dominika; na theluthi moja ni nchi ya Haiti. Nchi hii ina misitu ya mvua, milima mirefu, mikoko iliyoota kwenye maji, na majangwa. Mlima mrefu zaidi katika Jamhuri ya Dominika ni Pico Duarte, wenye urefu wa meta 3,175 juu ya usawa wa bahari. Maeneo mengi ya pwani yana fukwe maridadi zenye mchanga mweupe, na maeneo mengine ya nchi yana mabonde yenye rutuba, kama vile Bonde la Cibao.

Watu Wakazi wengi ni mchanganyiko wa watu wenye asili ya Ulaya na Afrika. Kuna jamii nyingi ndogo-ndogo; wengi wa wahamiaji hao wametoka nchini Haiti.

Lugha Kihispania ndiyo lugha rasmi.

Ndugu na dada wakifurahia ushirika

Kazi Uchimbaji wa madini, viwanda vya sukari, kahawa,  na tumbaku vimekuwa vyanzo vikuu vya mapato. Hivi karibuni, uchumi wa nchi hiyo umekua kwa sababu ya utalii na viwanda mbalimbali.

Hali ya hewa Kisiwa hicho kina hali ya hewa ya kitropiki, kila mwaka huwa na wastani wa nyuzi joto 25 za Selsiasi. Kiasi cha mvua kwa mwaka ni zaidi milimita 2,032 katika maeneo yenye milima ya kaskazini-mashariki na chini ya milimita 760 katika maeneo yenye ukame. Mara kwa mara kisiwa hicho hukumbwa na dhoruba ya upepo wa kitropiki na tufani.

Utamaduni Chakula kikuu hutia ndani mchele, maharagwe, na mboga. Wadominika pia hula vyakula vya baharini, matunda ya kitropiki, pilipili, na ndizi za kukaangwa. Baadhi ya vyakula hivyo hupatikana katika chakula maarufu zaidi kiitwacho La Bandera Dominicana (yaani, Bendera ya Dominika). Wakazi wa visiwani wanapenda mchezo wa besiboli, muziki, na kucheza dansi, hasa dansi iitwayo merengue. Gitaa huchezwa sana, vilevile ngoma, filimbi, na marimba.