MNAMO 1492, Christopher Columbus aligundua Ulimwengu Mpya, yaani, maeneo mapya yenye utajiri mwingi na maridadi sana. La Isla Española, au Hispaniola ni mojawapo ya visiwa alivyofikia, na sehemu kubwa ya kisiwa hicho ndiyo Jamhuri ya Dominika ya sasa. Hivi karibuni, maelfu ya wakazi wa Jamhuri ya Dominika wamejifunza jambo tofauti, yaani, ulimwengu mpya wenye uadilifu ambao utakuwa chini ya Ufalme wa Mungu. (2 Pet. 3:13) Historia ifuatayo inaonyesha jinsi ambavyo watu wenye mioyo minyofu wamejifunza jambo hilo lenye thamani sana.