MNAMO 1956, akina ndugu jijini Freetown waliwaonyesha watu sinema The New World Society in Action. Waliripoti hivi:

“Tulikodi ukumbi mkubwa zaidi jijini Freetown na kisha tukasambaza mialiko 1,000. Hatukuwa na hakika ni watu wangapi wangekuja. Nusu saa kabla ya sinema kuanza, ni watu 25 tu waliokuwa wamewasili. Dakika 15 zilizofuata, watu 100 zaidi walikuja. Baada ya muda mfupi viti vyote 500 vilikuwa vimejaa. Watu mia moja zaidi walikuwa tayari kusimama. Watu wengine 500 walisimama nje, kwani ndani hakukuwa na nafasi. Je, wangesubiri sinema hiyo ionyeshwe mara ya pili? Wakajibu, ‘ndiyo.’ Na hivyo ndivyo walivyofanya, walisubiri licha ya kwamba mvua ilikuwa ikinyesha!”

Kwa miaka mingi, zaidi ya watu 80,000 kotekote nchini Sierra Leone waliiona sinema hiyo na nyingine nyingi zenye kuvutia.