Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova

 SIERRA LEONE AND GUINEA

Vikundi vya Siri

Vikundi vya Siri

VIKUNDI vya siri vinapatikana kila mahali katika nchi za Afrika Magharibi na washiriki wake ni watu wa makabila, tamaduni, na lugha mbalimbali. Vikundi hivyo vinaratibu shughuli za kijamii, kielimu, na kisiasa za washiriki wao. Hata hivyo, lengo lao kuu ni dini. Vikundi vikubwa zaidi kuliko vingine vyote ni Poro (kwa ajili ya wanaume) na Sande (kwa ajili ya wanawake). * Kwa mfano, kikundi cha Poro kinahangakia sana “kudhibiti roho waovu na kuhakikisha kwamba roho hao wanapojihusisha katika masuala ya wanaume, inakuwa ni kwa manufaa ya wanaume hao.”Initiation, 1986.

Washiriki wapya wa kikundi cha Poro wanafundishwa kuhusu siri za ulimwengu wa roho na nguvu za uchawi, na kufanya tambiko la kuwaweka chale mwilini. Washiriki wapya wa kikundi cha Sande pia wanajifunza kuhusu ulimwengu wa roho na kwa kawaida wanawake hao hukeketwa, ingawa katika baadhi ya maeneo wameacha kukeketa.

Vikundi vingine vya siri vinadhibiti mwenendo wa kingono na kutibu ugonjwa wa akili na magonjwa mengine kwa kutumia dawa za waganga wa kienyeji. Wakati wa vita vya wenywewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone, kikundi kimoja cha siri kilidai kwamba washiriki wake hawawezi kuuawa kwa risasi. Haikuwa kweli.

Washiriki wanakatazwa kabisa kufichua maarifa na taratibu za kikundi. Mtu anayekiuka sheria na masharti ya kikundi cha siri anajihatarisha, kwani adhabu yake ni kifo.

^ fu. 3 Katika maeneo fulani, kikundi cha Sande kinajulikana pia kama Bondo.