Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 SIERRA LEONE NA GUINEA

Maelezo Mafupi Kuhusu Sierra Leone na Guinea

Maelezo Mafupi Kuhusu Sierra Leone na Guinea

Nchi Zote mbili zina maeneo yenye umajimaji au vidimbwi vya maji, nyanda za savana, nyanda za juu ambazo hutumika kwa kilimo, na milima mirefu. Mito mitatu mikubwa zaidi Afrika Magharibi inaanzia nchini Guinea—Mto Gambia, Niger, na Senegal.

Watu Wamende na Watemne ndiyo makabila makubwa zaidi miongoni mwa makabila 18 nchini Sierra Leone. Wakriowazao wa watumwa Waafrika waliowekwa huru—wanaishi katika maeneo yaliyo karibu na jiji la Freetown. Nchi ya Guinea ina zaidi ya makabila 30. Makabila makubwa zaidi ni Wafulani, Wamandingo, na Wasusu. *

Dini Asilimia 60 hivi ya raia wa Sierra Leone ni Waislamu; idadi kubwa ya wanaobaki ni wale wanaodai kuwa Wakristo. Karibu asilimia 90  ya watu nchini Guinea ni Waislamu. Pia, watu wengi katika nchi hizo mbili ni waumini wa dini za Kiafrika.

Lugha Kila kabila lina lugha yake. Lugha ya mawasiliano nchini Sierra Leone ni Krio, ambayo ni mchanganyiko wa Kiingereza, lugha za Ulaya, na za Afrika. Lugha rasmi nchini Guinea ni Kifaransa. Inakadiriwa kwamba karibu asilimia 60 ya watu katika kila nchi hawajui kusoma wala kuandika.

Kazi Watu wengi hulima mazao ya chakula kwa ajili ya familia zao. Karibu nusu ya mapato ya nchi ya Sierra Leone yanatokana na usafirishaji wa almasi nje ya nchi. Guinea ni mojawapo ya nchi zinazochimba kwa wingi zaidi madini ya boksiti (yanatokeza aluminiamu) duniani.

Chakula Msemo maarufu ni: “Ikiwa sijala wali, basi nimeshinda njaa!” Fufu (mihogo iliyochemshwa na kisha kupondwa-pondwa), mara nyingi huliwa pamoja na nyama, bamia au binda, na mchuzi.

Hali ya hewa Eneo la pwani lina joto na unyevunyevu. Kuna baridi kwenye maeneo ya nyanda za juu. Katika majira ya kiangazi, upepo mkali huvuma kutoka jangwa la Sahara ukiambatana na vumbi jingi. Upepo huo huvuma kwa siku nyingi, hupunguza kiasi cha joto na kufunika eneo lote kwa vumbi.

^ fu. 4 Makabila mengine yana jina zaidi ya moja.

 

SIERRA LEONE

GUINEA

UKUBWA WA NCHI (Kilometa za mraba)

27,699 (71,740 Kilometa za mraba)

94,926 (245,857 Kilometa za mraba)

IDADI YA WATU

6,092,000

11,745,000

IDADI YA WAHUBIRI MWAKA 2013

2,039

748

UWIANO, MHUBIRI MMOJA KWA WATU

2,988

15,702

HUDHURIO LA UKUMBUSHO MWAKA 2013

8,297

3,609