Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova

 SIERRA LEONE NA GUINEA

“Utakufa Kabla ya Mwaka Huu Kwisha”

Zachaeus Martyn

“Utakufa Kabla ya Mwaka Huu Kwisha”
  • ALIZALIWA 1880

  • ALIBATIZWA 1942

  • MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Alianza upainia alipokuwa na umri wa miaka 72.

ZACHAEUS hakufundishwa Biblia na mtu yeyote. Hata hivyo, baada ya kusoma kitabu Salvation na The Harp of God, akajua kwamba ameipata kweli.

Jumapili moja, mwaka 1941, Zachaeus alitoka asubuhi na mapema ili kwenda kuhudhuria mkutano wa Mashahidi kwa mara ya kwanza, ambao ulikuwa ukifanyika katika eneo lenye mteremko mkali umbali wa kilometa nane kutoka mahali alipoishi. Bila kujua mkutano ungeanza saa ngapi, aliwasili saa kadhaa mapema. Zachaeus alikaa na kungojea akina ndugu wawasili. Baada ya kuhudhuria mikutano kwa Jumapili tatu katika Jumba la Ufalme, akaliambia Kanisa la Anglikana lililokuwa katika eneo lao waondoe jina lake kwenye vitabu vyao.

Rafiki yake wa karibu, ambaye alikuwa mshiriki wa kanisa hilo, alimdhihaki akisema, “Mzee, ikiwa utaendelea kutembea hizo kilometa nane ukipanda na kushuka mlima huu kwenda kwenye jumba la watu hao, utakufa kabla ya mwaka huu kwisha.” Kwa miaka mitano aliendelea kumwona Zachaeus akipanda na kushuka mlima ule mara mbili kwa wiki. Kisha yule rafiki akafa ghafla! Miaka ishirini na tano baadaye, bado Zachaeus alikuwa mwenye nguvu.

Zachaeus aliendelea kumtumikia Yehova kwa uaminifu hadi alipokufa akiwa na umri wa miaka 97.