Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Sierra Leone na Guinea

Sierra Leone na Guinea

KARIBU miaka 500 hivi iliyopita, mti wa msufi uliota karibu na eneo ambalo Mto Sierra Leone unaingiza maji yake baharini. Kwa miaka 300 mti huo uliendelea kukua na wakati uleule misafara ya watumwa ikipita kando ya mti huo. Wafanyabiashara ya utumwa wakatili waliwasafirisha wanaume, wanawake, na watoto karibu 150,000 hadi nchi za ng’ambo kwenye masoko ya utumwa.

Mti wa Msufi wa kihistoria ulio jijini Freetown

 Mnamo Machi 11, 1792, mamia ya watumwa waliowekwa huru kutoka Marekani, walikusanyika chini ya mti huo ili kusherehekea kuwekwa kwao huru na kurudishwa Afrika. Siku hiyo wakaanzisha makazi ambayo yalikuwa alama ya matumaini yao—Freetown, yaani, mji huru. Watumwa waliowekwa huru waliendelea kuwasili Freetown, mwishowe jiji likawa na zaidi ya makabila 100 ya watu wenye asili ya Afrika. Raia hao wapya waliamua kuufanya ule Mti wa Msufi kuwa alama ya uhuru na matumaini.

Karibu miaka 100 hivi, Mashahidi wa Yehova nchini Sierra Leone wamekuwa wakiwafariji jirani zao kwa kuwajulisha tumaini la kupata uhuru mkubwa zaidi, yaani, “uhuru wenye utukufu wa watoto wa Mungu.” (Rom. 8:21) Uhuru huo utamaanisha kuwekwa huru kwa wanadamu kutoka katika utumwa wa dhambi na kifo, wakati Ufalme wa Mungu wa Kimasihi utakapoleta amani na Paradiso duniani.Isa. 9:6, 7; 11:6-9.

Katika miaka 50 iliyopita, ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Sierra Leone imekuwa ikisimamia pia kazi ya kuhubiri nchini Guinea. Nchi ya Guinea imekabiliana na misukosuko ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi, jambo ambalo limewafanya raia wengi wa nchi hiyo wakubali ujumbe wa Biblia unaogusa moyo.

Mashahidi wa Yehova nchini Sierra Leone na Guinea wametangaza habari njema chini ya vizuizi vingi. Vizuizi hivyo vinatia ndani hali ngumu ya maisha, umaskini uliokithiri, kutojua kusoma na kuandika, tamaduni zilizokita mizizi, migawanyiko ya kikabila, na jeuri mbaya sana. Habari ifuatayo inaonyesha wazi imani yao imara na ibada ya moyo wote ya watumishi hao washikamanifu wa Yehova. Tunatumaini kwamba maelezo yao yatachochea moyo wako na kuimarisha imani yako katika “Mungu anayetoa tumaini.”Rom. 15:13.

 

KATIKA SEHEMU HII

Maelezo Mafupi Kuhusu Sierra Leone na Guinea

Soma habari kuhusu nchi hizi, watu, dini, na lugha.

1915-1947 Siku za Mapema (Sehemu ya 1)

Mwaka 1915, mtumishi wa kwanza wa Yehova aliyebatizwa aliwasili jijini Freetown. Watu wengi walipendezwa na ujumbe wa Biblia.

1915-1947 Siku za Mapema (Sehemu ya 2)

Viongozi wa dini walipanga njama ya kuwanyamazisha watu wa Mungu, hata hivyo, Yehova ‘aliyageuza madhara yao yarudi juu yao.’

1915-1947 Siku za Mapema (Sehemu ya 3)

Kutaniko la Freetown likaanza ‘kushughulika sana na lile neno.’

“Utakufa Kabla ya Mwaka Huu Kwisha”

Zachaeus Martyn alitembea mara mbili kwa juma umbali wa kilometa nane, akipanda na kushuka mlima, ili ahudhurie mikutano ya Mashahidi wa Yehova. Ni nini kilichomthibishia kwamba alikuwa ameipata kweli ya Biblia?

Walimwita “Bible” Brown

William R. Brown alihubiri katika visiwa vingi vya Karibea na Afrika Magharibi. Soma habari hii uone ni kwa nini alihisi kwamba alikuwa amepewa mojawapo ya mapendeleo makubwa sana ambayo mwanadamu anaweza kupewa.

1945-1990 ‘Kuwaleta Wengi Kwenye Uadilifu’—Dan.12:3. (Sehemu ya 1)

Kazi ya kuhubiri ingefanywa kwa kiasi kikubwa. Wamishonari walitumwa ili wakachochee ukuzi.

Walitamani Kuiona

Mwaka 1956, sinema ‘The New World Society in Action’ ilionyeshwa jijini Freetown, Sierra Leone. Je, mtu yeyote angekuja kuiona?

1945-1990 ‘Kuwaleta Wengi Kwenye Uadilifu’—Dan.12:3. (Sehemu ya 2)

Mashahidi wa Yehova wanajulikana sana nchini Sierra Leone kuwa watu wanaoheshimu ndoa.

1945-1990 ‘Kuwaleta Wengi Kwenye Uadilifu’—Dan.12:3. (Sehemu ya 3)

Kwa nini wanasiasa wa kikundi cha Poro waliwasilisha mswada Bungeni ili kupiga marufuku kazi ya Mashahidi wa Yehova?

Vikundi vya Siri

Vikundi vya siri vimeathirije maisha ya wanaume na wanawake katika nchi za Afrika Magharibi?

1945-1990 ‘Kuwaleta Wengi Kwenye Uadilifu’—Dan.12:3. (Sehemu ya 4)

Makutaniko yaliendesha madarasa ya kuwafundisha watu kusoma kuandika ili kuwasaidia watu wakue kiroho. Kadiri watu walivyojua kusoma, ndivyo uhitaji wa kutafsiri ulivyoongezeka.

Beji Zilikuwa “Pasipoti” Zao

Wajumbe wa kusanyiko waliwezaje kuvuka mpaka na kuingia nchini Guinea ili wakahudhurie kusanyiko la wilaya ijapokuwa hawakuwa na hati za kusafiria, au pasipoti?

Yehova Amenisaidia

Jay Campbell, aliyeugua polio, alitaka kuhudhuria funzo la Biblia la kutaniko. Alisema kwamba angefika kwenye nyumba hiyo kwa kutumia vibao vyake alivyotumia kujikokota. Je, alifanikiwa?

1991-2001 ‘Tanuru ya Mateso’—Isa.48:10 (Sehemu ya 1)

Licha ya vita, Mashahidi wa Yehova walitoa msaada wa kimwili na wa kiroho kwa Mashahidi wenzao na watu wengine pia. Ni nini kilichowasaidia waonyeshe ujisiri na kubaki imara?

1991-2001 ‘Tanuru ya Mateso’—Isa.48:10 (Sehemu ya 2)

Vita vilipokuwa vikiendelea, Mashahidi wa Yehova “waliendelea kufundisha na kutangaza habari njema.”

Aliyekuwa Mwanajeshi Mtoto Awa Painia wa Kawaida

Mshiriki wa kikundi cha waasi alikumbuka jinsi alivyokaribishwa kwa uchangamfu alipohudhuria mkutano wa Mashahidi waYehova. Ni nini kilichomchochea afanye mabadiliko maishani?

Tuliwakimbia Wanajeshi Waasi

Kulikuwa na mauaji na machafuko katika mji wa Pendembu, kwa nini baadhi ya Mashahidi hawakuuawa vita vilipozuka mwaka 1991?

Mtu wa Mnara wa Mlinzi

Shahidi wa Yehova mmoja alikuwa mjumbe wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Aliwezaje kubeba barua na baadhi ya vitu kutoka jijini Freetown hadi Conakry, nchini Guinea?

Kitu Bora Zaidi Kuliko Almasi

Tamba Josiah alifanya kazi katika migodi ya almasi kabla ya kuwa Shahidi wa Yehova. Kwa nini alihisi kwamba alipata kitu bora zaidi kuliko almasi?

Mwaka 2002-2013 Ongezeko la Karibuni (Sehemu ya 1)

Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, makutaniko yalianzishwa, na mapainia wa pekee walitumwa kwenye maeneo ambayo yalikuwa na Mashahidi wachache.

2002-2013 Ongezeko la Karibuni (Sehemu ya 2)

Leo, Mashahidi wa Yehova katika nchi hizo mbili wanaamini kwamba bado kuna watu wengi zaidi ambao watakubali habari njema za Ufalme.

Nimeazimia Kumtumikia Yehova

Phillip Tengbeh na mke wake walikimbia ili kuokoa maisha yao wakati wanajeshi waasi walipouvamia mji walioishi, Koindu. Walipokuwa wakiishi katika kambi hizo, walisaidia kujenga Majumba matano ya Ufalme.

Ninaipenda Sana Nchi ya Sierra Leone

Cindy McIntire ametumikia akiwa mmishonari barani Afrika tangu mwaka 1992. Anaeleza sababu inayomfanya afurahie kuhubiri hasa nchini Sierra Leone.