TAZAMA
Maandishi
Picha

Pakua:

 1. 1. Kazi ya Ufalme leo hata zamani,

  Huandaa neno lako kweli na mengine.

  Na mtumwa wako hutuangazia nuru

  Huwatuma wachungaji wanaonipenda.

  Ninatazamia kusanyiko kwa hamu,

  Na mwishowe nitasema, “Lilikuwa bora!”

  Mikutanoni nahisi unavyotujali

  Twajifunza kuhubiri pia kufundisha.

  (KORASI)

  Twastaajabia,

  Kazi za Ufalme wako.

  Twathamini sana.

  Tunapokujua wewe imani yakua.

  Twatazamia baraka nyingi za Ufalme.

 2. 2. Tuna pendeleo kufanya kazi nawe,

  Utumishi wetu ni wonyesho wa upendo.

  Tuna ufahamu na amani ya akili,

  Twajifunza Neno lako, Jinsi ya kuishi.

  Na nyimbo tamu zagusa hisia zangu

  Ibada ya familia ni muhimu pia.

  Tuna umoja licha ya lugha tofauti.

  Kwa kweli tuna undugu wa pekee sana.

  (KORASI)

  Twastaajabia,

  Kazi za Ufalme wako.

  Twathamini sana.

  Tunapokujua wewe imani yakua.

  Twatazamia baraka nyingi za Ufalme.