TAZAMA
Maandishi
Picha

Pakua:

 1. 1. N’likuwa gizani; maswali mengi,

  Umenifundisha, nina hamu.

  Mafundisho, nayapenda.

  Maswali yangu yalijibiwa.

  Wasiwasi ukaondoka wote.

  Shaka zangu zikaisha.

  (KORASI)

  Si rahisi kugeuka!

  Imani ina nguvu.

  Hata kukiwa na magumu,

  Imani hushinda.

  Ina nguvu.

 2. 2. N’nayojifunza, nayahubiri.

  Tamaa ninayo, nina hamu.

  N’ko tayari,

  Nikahubiri.

  Imani yawaka, moto wa moyoni.

  Lazima niuchochee uwake,

  Sikuzote. Sikuzote.

  (KORASI)

  Kazi ngumu, ya kufanya.

  Hata hivyo, najua:

  Hata kukiwa na magumu,

  Imani hushinda.

  Ina nguvu.

  (DARAJA)

  Siku mbovu, mbaya, huvunja moyo.

  Nayo sala hujenga, kaahidi Yehova:

  “Ewe ukinitumaini,

  Nitakupa wewe nguvu,

  Ulipojaribiwa,

  Nilikuwa nawe!”

  (KORASI)

  Kazi ngumu, ya kufanya

  Hata hivyo, najua,

  Hata kukiwa na magumu,

  Imani hushinda.

  (KORASI)

  Ninajua. Sina shaka.

  Imani hushinda.

  Hata kukiwa na magumu,

  Imani hushinda,

  Ina nguvu.