Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Mwimbieni Yehova—Nyimbo Mpya

 Wimbo Na. 154

Tutaendelea Kuvumilia

Tutaendelea Kuvumilia

Pakua:

(Mathayo 24:13)

 1. Yesu asema

  Tuvumilie magumu.

  Alikazia shangwe

  ya mambo yajayo.

  Ahadi ya Mungu,

  alitafakari.

  (KORASI)

  Tuwe wavumilivu.

  Tulinde imani.

  Kwa kuwa atupenda,

  tutavumilia hadi mwisho.

 2. Japo maisha

  yamejawa na uchungu;

  Sisi twaona,

  uzima wenye furaha.

  Imara, thabiti,

  Tutavumilia.

  (KORASI)

  Tuwe wavumilivu.

  Tulinde imani.

  Kwa kuwa atupenda,

  tutavumilia hadi mwisho.

 3. Hatufi moyo

  Wala hatutaogopa.

  Tutadumisha

  uaminifu kwa Mungu.

  Imara, tudumu,

  Siku I karibu.

  (KORASI)

  Tuwe wavumilivu.

  Tulinde imani.

  Kwa kuwa atupenda,

  tutavumilia hadi mwisho.