Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Mwimbieni Yehova—Nyimbo Mpya

 Wimbo Na. 137

Tupe Ujasiri

Tupe Ujasiri

Pakua:

(Matendo 4:29)

 1. Tuhubiripo Ufalme,

  Na jina kutangaza,

  Ni wengi wanatupinga

  Na kutuaibisha.

  Hatuogopi watu,

  Ni wewe tunayetii.

  Twasali tupe roho yako;

  Yehova, tusikilize.

  (KORASI)

  Tupe ujasiri Baba;

  Ili tushinde woga.

  Tupe uhodari Baba

  Tuweze kuhubiri.

  Har-magedoni karibu,

  Lakini kabla ifike,

  Tupe ujasiri Baba.

  Twakuomba.

 2. Kumbuka sisi mavumbi,

  Basi twaogopeshwa.

  Tunaamini ahadi

  Utatusaidia.

  Angalia vitisho

  Vya wanaotunyanyasa.

  Tupe sote uvumilivu

  Tuseme kwa ujasiri.

  (KORASI)

  Tupe ujasiri Baba;

  Ili tushinde woga.

  Tupe uhodari Baba

  Tuweze kuhubiri.

  Har-magedoni karibu,

  Lakini kabla ifike,

  Tupe ujasiri Baba.

  Twakuomba.