TAZAMA
Maandishi
Picha

(1 Nyakati 29:16)

 1. 1. Ni pendeleo, Ee, Yehova,

  Kukujengea mahali!

  Twakutolea kwa shukrani.

  Heshima na sifa kwako.

  Vyote tunavyokupatia,

  Vimetoka kwako wewe.

  Kazi, stadi, na mali zetu,

  Twatoa kwa moyo wote.

  (KORASI)

  Tunakupa jengo hili,

  Liitwe jina lako.

  Twaliweka wakfu kwako;

  Lipokee, twaomba.

 2. 2. Wastahili heshima, Baba,

  Uzidi kupata sifa.

  Utukufu upande juu.

  Wengi wajiunge nasi.

  Pawe mahali pa ibada.

  Tutapatunza vizuri.

  Watu wapate kukujua,

  Na kazi isonge mbele.

  (KORASI)

  Tunakupa jengo hili,

  Liitwe jina lako.

  Twaliweka wakfu kwako;

  Lipokee, twaomba.