TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 127:1)

 1. 1. Yehova twasimama,

  Mbele zako leo hii.

  Umeibariki

  Kazi yetu ya ujenzi.

  Sasa tunaliona,

  Jengo linalopendeza.

  Na mioyo yetu,

  Imejawa na shukrani.

  (KORASI)

  Ee, Yehova, ni pendeleo,

  Kulijenga jengo hili.

  Twataka kukutumikia sikuzote,

  Na kukusifu kwa yote.

 2. 2. Tuna furaha nyingi,

  Tumepata marafiki!

  Hatutasahau,

  La hasha​—⁠hadi milele!

  Yehova roho yako,

  Imekuwa juu yetu.

  Wastahili sifa;

  Jina lako litukuzwe!

  (KORASI)

  Ee, Yehova, ni pendeleo,

  Kulijenga jengo hili.

  Twataka kukutumikia sikuzote,

  Na kukusifu kwa yote.