TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 25:4)

 1. 1. Tumekutanika, Yehova Mungu;

  Mwaliko wako twakubali.

  Na Neno lako latuangazia,

  Njia zako tunafundishwa.

  (KORASI)

  Nifundishe njia zako wewe;

  Nieleweshe hekima yako.

  Unitembeze katika kweli.

  Nami nipende sheria yako.

 2. 2. Hekima yako haina kifani;

  Hukumu zako ni za haki.

  Neno lako ni la ajabu sana.

  Maneno yako yanadumu.

  (KORASI)

  Nifundishe njia zako wewe;

  Nieleweshe hekima yako.

  Unitembeze katika kweli.

  Nami nipende sheria yako.