Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 WIMBO NA. 8

Yehova Ni Kimbilio Letu

Chagua Rekodi ya Sauti
Yehova Ni Kimbilio Letu
TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 91)

 1. 1. Yehova, kimbilio,

  Ndiye twatumai.

  Yeye ni ngome yetu;

  Kwake twajificha.

  Mungu atatuokoa,

  Kamwe hatutaogopa.

  Yehova, kimbilio,

  Kwa waadilifu wote.

 2. 2. Maelfu waanguka,

  Kando yetu sisi.

  Kati ya wa’dilifu,

  Kuna usalama.

  Hatuna hofu moyoni,

  Dhara halitatupata.

  Chini ya mbawa zake,

  Yehova atatulinda.

 3. 3. Yehova yuko nasi,

  Hatutajikwaa.

  Vitisho, hatuhofu,

  Hatubabaiki.

  Mwana-simba hatuhofu;

  Nyoka tutamkanyaga.

  Yehova, kimbilio,

  Atuongoza milele.