Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 WIMBO NA. 78

Kufundisha Neno la Mungu

Chagua Rekodi ya Sauti
Kufundisha Neno la Mungu
TAZAMA
Maandishi
Picha

(Matendo 18:11)

 1. 1. Tuwafundishapo watu,

  Neno lake Mungu.

  Baraka tunazopata,

  Hazina kifani.

  Tunamwiga Kristo Yesu,

  Alivyofundisha.

  Tungependa tufundishao

  Wawe rafikize.

 2. 2. Tukiwa walimu stadi

  Tuweke mfano;

  Waone unyofu wetu,

  Tuangaze nuru.

  Tuchunguze Maandiko,

  Tuyatafakari.

  Tujifunze ili tufunze

  Na wengine pia.

 3. 3. Yehova hutuwezesha,

  Kufundisha Neno.

  Tukimwomba msaada,

  Atatusikia.

  Twalipenda Neno Lake,

  Tunalithamini.

  Tuwapende tuwafunzao

  Wajiunge nasi.