TAZAMA
Maandishi
Picha

(Isaya 6:8)

 1. 1. Leo watu hudhihaki,

  Jina tukufu la Mungu.

  Wasema “Hakuna Mungu! ”

  Eti Mungu ni dhaifu.

  Nani atamtetea,

  Na kulitakasa jina?

  (KORASI YA 1)

  ‘Bwana, Mimi hapa! N’tume.

  Nitakusifu daima.

  Ni pendeleo kubwa sana.

  Bwana nitume mimi.’

 2. 2. Hawamwogopi Yehova

  Wadai anakawia.

  Sanamu waziabudu.

  Kaisari wamwabudu.

  Nani atatoa onyo,

  Kuhusu vita vya Mungu?

   (KORASI YA 2)

  ‘Bwana, Mimi hapa! N’tume.

  Nitawaonya waovu.

  Ni pendeleo kubwa sana.

  Bwana nitume mimi.’

 3. 3. Wapole wanaugua,

  Mbona maovu yazidi?

  Kwa unyofu watafuta

  Ukweli wenye amani.

  Nani atawafariji,

  Upole wautafute?

  KORASI YA 3)

  ‘Bwana, Mimi hapa! N’tume.

  Nitawafunza wapole.

  Ni pendeleo kubwa sana.

  Bwana nitume mimi.’