Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 WIMBO NA. 66

Tangaza Habari Njema

Chagua Rekodi ya Sauti
Tangaza Habari Njema
TAZAMA
Maandishi
Picha

(Ufunuo 14:6, 7)

 1. 1. Kusudi la Yehova ametangaza,

  Yale Ufalme utayatekeleza.

  Yehova kwa rehema atubariki,

  Kuangamiza wanadamu hataki.

  Kristo taji Yehova amemvika.

  Na wakati wa utawala umefika.

  Bibi-harusi wa Kristo yu tayari,

  Kundi dogo la wasio na dosari.

 2. 2. Habari njema leo tunatangaza.

  Twataka wote wazisikie sasa.

  Na malaika wanatutegemeza,

  Kazi ya Ufalme kuitekeleza.

  Tuna pendeleo kubwa leo hasa,

  Jina la Yehova Mungu kulitakasa.

  Tumependelewa kuwa Mashahidi.

  Kutangaza habari njema tuzidi.