TAZAMA
Maandishi
Picha

(Waebrania 6:1)

 1. 1. Songa mbele, fikia ukomavu!

  Angaza kote nuru ya habari njema.

  Boresha ustadi wako shambani,

  Mtegemee Mungu.

  Sote twaweza kuhubiri.

  Yesu aliweka mfano.

  Mwombe Mungu akupe nguvu zake,

  Usimame imara.

 2. 2. Songa mbele, uwe na ujasiri!

  Tangazia watu wote habari njema.

  Tumsifu Yehova kwa furaha,

  Tuhubiripo kote.

  Adui wajapotutisha.

  Usihofu; tangaza kote,

  Kwamba Ufalme watawala sasa.

  Hubiri kwa bidii.

 3.  3. Songa mbele, wasaidie wapya,

  Uwe na ustadi,

  kazi ni nyingi sana.

  Roho ya Mungu na ikuchochee.

  Nawe upate shangwe.

  Upendezwe na watu wote.

  Usikose kuwarudia.

  Uwasaidie wasonge mbele.

  Ukweli uangaze.