TAZAMA

(Mathayo 13:1-23)

 1. 1. Twaishi siku za mavuno,

  Pendeleo kubwa sana.

  Mashamba ya ngano tayari,

  Twashiriki kuyavuna.

  Kristo ameweka mfano;

  Anaelekeza kazi.

  Tuna pendeleo kubwa sana,

  Tufanye kazi ya Bwana.

 2. 2. Mungu, jirani, tukipenda,

  Tutachochewa kutenda.

  Tuna kazi muhimu sana,

  Mwisho u karibu sana.

  Tuzidipo kufanya kazi,

  Tutakuwa na furaha.

  Kazi ya Ufalme tushiriki,

  Mungu atatubariki.