TAZAMA
Maandishi
Picha

(Isaya 43:10-12)

 1. 1. Watu wana miungu,

  Ya miti na ya mawe.

  Nao hawajui,

  Mungu wa kweli.

  Miungu yote hiyo

  Haioni yajayo.

  Wala haina mashahidi,

  Kwa kuwa ni ya uwongo.

  (KORASI)

  Mungu wetu wa kweli,

  Hutimiza ahadi.

  Tu Mashahidi wa Yehova;

  Twasema bila woga.

 2. 2. Jina lake Yehova,

  Twalitangaza kote.

  Ufalme wa Mungu,

  Twautangaza.

  Watu wawekwe huru

  Na kweli za Yehova.

  Wajiunge nasi kuimba,

  Sifa za Yehova Mungu.

  (KORASI)

  Mungu wetu wa kweli,

  Hutimiza ahadi.

  Tu Mashahidi wa Yehova;

  Twasema bila woga.

 3.  3. Kushuhudia jina,

  Huondoa lawama.

  Huonya waovu,

  Wenye dhihaka.

  Wakirudi kwa Mungu,

  Atawakaribisha.

  Shangwe na amani twapata

  Na uzima wa milele.

  (KORASI)

  Mungu wetu wa kweli,

  Hutimiza ahadi.

  Tu Mashahidi wa Yehova;

  Twasema bila woga.